WANACHAMA WATAKIWA KUWAJIBIKA ENEO LA KAZI- VIDEO.



Ben Komba/Pwani-Tanzania/07-11-2014
Wafanyakazi wa  wametakiwa kuwajibika katika maeneo ya kazi ili kuwezesha vyama vya wafanyakazi kuwa na nguvu ya kisheria na maadili wakati wa kuwatetea wanapokutwa na matatizo eneo la kazi.

Mwenyekiti wa Tawi la chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa-TALGWU- la Halmashauri ya mji, BW.MOHAMED MAHINGIKA amesema hayo akifungia semina kwa viongozi wapya wa matawi ya chama hicho katika halmashauri ya mji wa Kibaha.

BW.MAHINGIKA amefafanua kwa wafanyakazi kuheshimu wajibu na taratibu za kazi kutasaidia katika kuvipa nguvu vyama vyao vya wafanyakazi katika kuwatetea wanapokumbwa na matatizo mbalimbali ya kikazi.

BW.MAHINGIKA ameongeza kuwa matawi ambayo yamepata viongozi wapya ni kutoka tawi la kituo cha afya mkoani na zahanati ya Mwendapole, aidha amewasisitizia wanachama wa TALGWU kutanguliza mbele upendo na masikiklizano sehemu ya kazi.

Naye Kaimu Katibu wa TALGWU Mkoa wa Pwani, BIBI.AMINA DARABU amesema kuwa Chama chochote Duniani kinasimama kwa kuwa na wanachama ikiwa pamoja na kulipa ada ya uendeshaji wa chama.

Ameongeza Kaimu katibu huyo wa TALGWU Moa wa Pwani, BI.DARABU amewataka viongozi wapya kutoa taarifa kwa kila kinachoendelea maeneo ya kazi kuripoti katika ofisi yake ili yapatiwe ufumbuzi stahili.
END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA