WAFANYAKAZI WATAKIWA KUWAJIBIKA MAENEO YA KAZI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/07-11-2014
Wafanyakazi
wa wametakiwa kuwajibika katika maeneo
ya kazi ili kuwezesha vyama vya wafanyakazi kuwa na nguvu ya kisheria na
maadili wakati wa kuwatetea wanapokutwa na matatizo eneo la kazi.
Mwenyekiti wa
Tawi la chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa-TALGWU- la Halmashauri ya
mji, BW.MOHAMED MAHINGIKA amesema hayo akifungia semina kwa viongozi wapya wa
matawi ya chama hicho katika halmashauri ya mji wa Kibaha.
BW.MAHINGIKA
amefafanua kwa wafanyakazi kuheshimu wajibu na taratibu za kazi kutasaidia
katika kuvipa nguvu vyama vyao vya wafanyakazi katika kuwatetea wanapokumbwa na
matatizo mbalimbali ya kikazi.
BW.MAHINGIKA
ameongeza kuwa matawi ambayo yamepata viongozi wapya ni kutoka tawi la kituo
cha afya mkoani na zahanati ya Mwendapole, aidha amewasisitizia wanachama wa
TALGWU kutanguliza mbele upendo na masikiklizano sehemu ya kazi.
Naye Kaimu
Katibu wa TALGWU Mkoa wa Pwani, BIBI.AMINA DARABU amesema kuwa Chama chochote
Duniani kinasimama kwa kuwa na wanachama ikiwa pamoja na kulipa ada ya
uendeshaji wa chama.
Ameongeza Kaimu
katibu huyo wa TALGWU Moa wa Pwani, BI.DARABU amewataka viongozi wapya kutoa
taarifa kwa kila kinachoendelea maeneo ya kazi kuripoti katika ofisi yake ili
yapatiwe ufumbuzi stahili.
END.
Comments
Post a Comment