BRITISH COUNCIL YASAIDIA VITABU SEKONDARI YA MWAMBISI-VIDEO



Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-11-2014
Mkuu wa wilaya ya Kibaha BIBI. HALIMA KIHEMBA amepokea msaada wa vitabu vya kufundishia vya masomo ya Sayansi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6 kutoka shule ya LATYMER ya Nchini Uingereza kwa shule ya sekondari ya Kata ya Mwambisi katika suala zima la kukuza mshikamano kati ya shule hizo mbili.

BIBI.KIHEMBA ameongeza kuwa msaada huo umekuja katika kipindi mwafaka wakati serikali ipo katika vuguvugu la ujenzi wa maabara katika kila shule ya sekondari nchini  kwa lengo la kuimarisha utoaji elimu katika masomo ya sayansi.

Amesisitiza kuwa ni jambo la muhimu kuzingatia usalama wa vitu ambvyo vimetolewa ili viweze kuwasaidia na wengine ambao watabahatika kusoma shuleni hapo.

Aidha Mkuu wa wilaya Kibaha BIBI.KIHEMBA ametoa ushauri kwa uongozi wa shule hiyo kuanzisha na maabara ya kompyuta ili kupanua wigo wa utoaji elimu shuleni hapo.

Naye mwakilishi kutoka BRITISH COUNCIL, BI.LILIAN MSUYA akikabidhi vifaa hivyo amesema wamekuwa wakishirikiana na shule ya sekondari Mwambisi katika kuhakikisha Walimu wanapatiwa mbinu bora za ufundishaji wa masomo ya Sayansi.

BI.MSUYA amesema toka kuanzishwa kwa ushirikiana huo baadhi ya Walimu wameshatembelea shule ya LATYMER ambayo ipo nchini Uingereza ili kwenda kujifunza kutoka kwa wenzao.

Ameweka wazi mafanikio ambayo wanategemea shule ya sekondari ya MWAMBISI kuyapata ni pamoja  na kujengewa uwezo na kuwa shule ya mfano katika utoaji elimu mkoa wa Pwani.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA