MABONDIA KUPAMBANA PWANI NOVEMBA 27 2014-VIDEO



Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-11-2014

Kampuni ya GEORGE PROMOTION imeandaa Pambano la ngumi kukata na shoka kati ya Bondia anayechipukia katika mchezo huo mkoa wa Pwani, ZUMBA KUKWE na Bondia mkongwe nchini SWEET KALULU katika  pambano ambalo litafanyika kesho Novemba 27 kwenye ukumbi wa Kontena mjini Kibaha.

Muandaaji wa mpambano huo, GEORGE NANGAI amesema kabla ya pambano hilo lisilo la ubingwa kutakuwepo na mapambano ya utangulizi ambapo KISOO SOLI atapambana na ISSA NAMPECHECHE, RAMA MAX atapambana na MUSTAPHA DOTTO.

Bw. NANGAI amebainisha kuwa lengo la kuaanda mpambano huo ni kunyanyua mchezo wa ngumi katika Mkoa wa Pwani, kwa kutoa fursa kwa vijana kujiajiri katika mchezo huo.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA