WAFANYABIASHARA SOKO LA MAILIMOJA WANATAKA WATHAMINIWE


Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/16/2016 8:42:21 AM
Wafanyabiashara katika soko la Mailimoja halmashauri ya mji wa Kibaha wameitaka serikali kuwalinda ili kuepuka changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wao wa majukumu yao ya kila siku.

Mratibu wa wafanyabiashara nchini, BW.ALLY NDAUKA ameongea hayo katika mkutano wa wafanyabiashara wa soko la Maili moja ambapo amesema wafanyabiashara wadogo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi.

BW.NDAUKA ameongeza kuwa wafanyabiashara wamekuwa wakifilisiwa kutokana na uwepo wa sheria stukizi ambazo mara nyingi huwasababishia wafanyabiashara hasara na hasa ikizingatiwa wafanyabiashara hao wanaendesha biashara zao kwa mikopo.

Naye mmoja wa wafanyabiashara sokoni hapo, BW.RAMADHAN NGOWO amepinga kufanyika kikao hicho kutokana na kukosekana kwa Mkurugenzi wa mji na afisa biashara wahalmashauri ya mji wa Kibaha.

Bw .NGOWO amefafanua wamekuwa wakilipishwa ushuru mbalimbali kinyume cha taratibu kiasi kwamba zinachangia kudumaa kwa biashara zilizopo ametoa mfano, ushuru wa halmashauri ni shilingi 300 lakini wakusanya ushuru wanatoza shilingi 500, hali ambayo inawaleta sintofahamu wafanyabiashara.


END. 

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA