MKUU WA WILAYA BAGAMOYO AZUIA MKUTANO WA WAFUGAJI WA KIMASAI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/9/2016 1:02:57 PM
Mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo, BW.MAJID MWANGA amelazimika kusimamisha mkutano wa watu wa
jamii ya Kimasai kwa madai ya kutokuwa na kibali chenye kuwawezesha kufanya
mkutano huo.
Kwa mujibu
wa Mkazi wa kijiji cha wafugaji Chamakweza BIBI REHEMA LAINI amesema sababu ya
kukusanyika kwao ni kupokonywa eneo lao kwa lengo la kuanzisha mipango miji
ilihali ikijulikana wazi mifugo haiwezi kuishi mjini.
BIBI LAINI
ameongeza jamii yao imekuwa inanyanyasika sana kama wafugaji na hasa
ikizingatiwa mpango bora wa matumizi ya ardhi ambao ulikuwa na lengo la
kuainisha matumizi ya ardhi.
Mkazi mwingine
wa Chamakweza BW.WILSON OLDONYO amesema tatizo kubwa ambalo wanakabiliana nalo
ni kuanzishwa mpango wa mipango miji kitu ambacho walikigomea kiasi cha kususia
uchaguzi mkuu uliopita na amebainisha kuwa kijiji cha Chamakweza kimepewa hadhi
ya kuwa kijiji cha wafugaji toka mwaka 1975.
Ameongeza kuwa
walijaribu kufanya jitihada ya kubadilisha mpango huo, na wakiagizwa wasubiri
majibu lakini mwisho wa siku waliambiwa warudi kijijini ambapo wakafanye mpango
kijiji hicho kiwe Kata.
END.
Comments
Post a Comment