VIDEO- WENYE MDOMO SUNGURA KUFANYIWA UPASUAJI BURE MKOANI KAGERA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/7/2016 7:11:52 AM
Wananchi wa
Mkoa wa Kagera kupitia taasisi isiyo ya kiserikali ya THE MIGHTY FORTERESS
FOUNDATION ya Uholanzi wamebahatika kupata huduma ya upasuaji ya watu wenye
matatizo ya mdomo sungura katika jitihada za kutoa huduma za afya kwa wahitaji.
Mwakilishi
wa shirika hilo nchini, Mchungaji GERVAS MASANJA amesema wameamua kutoa huduma
hiyo kutokana na kuwepo kwa wanajamii wenye tatizo hilo na kutoa fursa kwao kutumia
nafasi hii adimu ya kupata upasuaji ambayo ingewagharimu fedha nyingi.
Mwakilishi
huyo MCH.MASANJA amesema kwamba watashirikiana na wataalamu bingwa wa upasuaji
kutoka nchini Holland wanaojulikana kama INTERPLAST HOLLAND pamoja na madaktari
bingwa wa hapa nchini na zoezi hilo linatarajiwa kufanyika katika hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Kagera kati ya tarehe
26 machi mpaka tarehe 1 april , Machi 20 mpaka 25 upasuaji huo utafanyika katika hospitali ya
Ndolage Bukoba.
END.
Comments
Post a Comment