MRADI WA MAJI KATA YA PANGANI KIBAHA NI JIPU
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/25/2016 12:44:42 PM
Wananchi
katika Kata ya Pangani wameilalamikia halmashauri ya mji wa Kibaha kwa
kushindwa kutekeleza mradi wa maji ambao umegharimu zaidi ya shilingi milioni mia tano ambazo inasemekana
zimetumika kinyume cha taratibu na kusababisha mradi kuwa chini ya kiwango
stahili.
Aliyekuwa Mwenyekiti
wa kamati ya watumiaji maji, BW.REGINALD MUSHI ambaye amesema mradi huo wa maji katika Kata ya Pangani umekuwa
ukikabilwa na changamoto mbalimbali za utekelezaji.
BW.MUSHI
amebainisha kuwa mabomba yaliyotumika ni REJECT kiasi kwamba maji
yalipofunguliwa mabomba hayo yakaanza kupasuka hovyo na kusababisha mradi
kushindwa kufikia malengo ya kuwafikishia wananchi maji ya bomba.
BW.MUSHI
ameongeza kuwa kilipofika kipindi cha kununua vifaa kamati ya watumiaji maji
ikawekwa kando na maofisa wa halmashauri ndio wliokwenda kununua mabomba hayo,
Kwa makadirio yake anasema mradi huo utekelezaji wake una ubadhirifu kwa shilingi
milioni 150 tu zingetosha kukamilisha mradi huo.
Vox 1-REGINALD
MUSHI
VOX 2-CHUKI
HASSAN Aliyekuwa mjumbe wa kamati ya maji kabla ya fedha kuingizwa
Vox
3-mwananchi
Naye diwani
wa Kata ya Pangani, BW.AUGUSTINO MDACHI ameelezea dhiki kubwa ambayo wananchi
wa Kata yake wanaipata kutokana na kukosa maji kwa takriban miezi miwili sasa
kutokana na mradi kushindwa kukidhi mahitaji ya upatikanaji maji.
END.
Comments
Post a Comment