VIDEO-KATA YA PANGANI MJINI KIBAHA YA MFANO KTK POLISI JAMII KIMKOA


Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/22/2016 3:13:38 PM
Katika kuimarisha ulinzi na usalama wa Mtaa wa Pangani halmashauri ya mji wa Kibaha umefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa wimbi la uhalifu ambalo lilikuwa limetawala katika mtaa huo.

Akisoma taarifa ya kikosi cha Polisi jamii kwa mgeni rasmi mara baada ya kuhitimu mafunzo ya ukakamavu mmoja wa maaskari wa Polisi jamii Kata ya Pangani, BI.ASHA KIRUMBI amesema toka kuanzishwa kwa ulinzi shirikishi jamii kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kupunguza uhalifu ambao ulikuwa unajitokeza mara kwa mara.

BI.KIRUMBI ameongeza kuwa kabla ya kuanza kwa ulinzi shirikishi jamii walikuwa wakikabiliwa na vitendo mbalimb ali vya uhalifu ikiwa pamoja na mauaji na ukabaji, vitendo ambavyo kwa sasa vimedhibitiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na juhudi ambazo zimefanywa na Jeshi la Polisi mjini Kibaha.

BI.KIRUMBI amechukua hatua kumpongeza Polisi Kata ya Pangani KOPLO SILVERY MUJUNI ambaye amewawezesha kwa kuwapa moyo na mbinu mbalimbali za kudhibiti uhalifu katika maeneo yanayowazunguka yenye mitaa  tisa hivyo amelitaka Jeshi la Polisi kumfikiria askari huyo kutokana na jitihada zake alizoonyesha.

Naye Inspekta msaidizi wa Jeshi la Polisi FANUEL MILINGA akijibu risala ya washiriki wa gwaride la Polisi hao jamii, amesema kwa upande wa Jeshi la Polisi watajitahidi kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wao wa majukumu ya kila siku.

Kata ya Pangani ni iliyopo katika halmashauri ya mji wa Kibaha imeshawahi kutunukiwa cheti cha ubora katika utoaji wa huduma za Polisi ulinzi shirikishi jamii mkoani Pwani na hivyo kuchukuliwa kama ni moja ya Kata ya mfano nchini katika suala zima la kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.

END 

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA