VIDEO-MWENYEKITI WA USHIRIKA ASIMAMISHWA KWA KUJIKOPESHA FEDHA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/24/2016 10:30:47 AM
Mwenyekiti
wa ushirika wa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji Ruvu katika
halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo amesimamishwa uongozi kutokana na kile
kinachodaiwa amejikopesha fedha za ushirika huo.
Kaimu mrajis
msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Pwani, BW.HIJA YANGE amesema Mwenyekiti
huyo wa ushirika wa umwagiliaji BW.
ERASTO MWAMKINGA inasemekana alijikopesha fedha hizo katika kipindi cha Desemba
mwaka jana bila kufuata utaratibu wa vyama vya ushirika.
BW.NYANGE
amewataka wanachama kutafakari hatua gani ambazo watzichukua dhidi ya
Mwenyekiti huyo na wenzie wengine wawili ambao walishiriki katika kutia saini
na kuwezesha kuchotwa kwa fedha takriban milioni 26.
VOX 1-
IBRAHIM NINDI Afisa ushirika aliyechunguza
Vox – 2-HIJA
YANGE-MRAJIS MSAIDIZI USHIRIKA PWANI
Hata hivyo
katika hatua nyingine, Makamu mwenyekiti wa Ushirika huo wa kilimo cha mpunga
kwa njia ya umwagiliaji amewaambia wanaushirika huo kuwa mpaka sasa Mwenyekiti
Mwamkinga ameshaanza kulipa fedha hizo.
Wakati kikao
hicho kikifanyika Mwenyekiti huyo hakuwepo kutokana na kukabiliwa na udhuru.
END
Comments
Post a Comment