VIDEO-WANANCHI SOGA WALALAMIKIA VIONGOZI WA KIJIJI NA DIWANI KUUZA ARDHI KINYEMELA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/6/2016 10:36:21 AM
Umoja wa
wakulima Soga umelalamikia hatua ya uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha
kutumia nguvu kuwatoa eneo ambalo wao wamaeamua kulitumia baada ya kukaa muda
mrefu na kugeuka shamba pori.
Wakizungumza
na mwandishi wa Habari hizi, mmoja wa wakazi wa eneo hilo maarufu kama
Kazamoyo, BW.MOHAMED CHETO amesema kuwa wao kama wananchi walianza harakati za
kutaka kulitumia eneo hilo mara baada ya kuona ni muda mrefu limeachwa ilihali
wao wana dhiki ya ardhi.
BW.CHETO
amebainisha kuwa mara baada ya wao kuvamia ambaye anadaiwa kuwa mmiliki
BW.JAHANGIR POPTAN alifungua kesi katika mahakama ya mwanzo Mailimoja
akimshataki BW.YUSUPH KILIMA na wenzake 11, Ambapo hata hivyo mahakama hiyo
ikaamuru akafungue kesi katika baraza la ardhi la wilaya na kuwaachia huru wote
ambao walishtakiwa.
Lakini baada
ya BW.JAHANGIR POPTAN kushindwa katika shauri hilo baadhi ya viongozi wa kijiji
na Kata wamekuwa wakitumia nafasi zao kuwabugudhi wananchi kwa kutumia Jeshi la
Polisi kuwafukuza, na wao wakiendelea kuuza kinyemela eneo hilo kwa maslahi
binafsi.
Naye katibu
wa umoja wa wakulima Soga, BW.OTHMAN RASHID amesema wao mpaka sasa
wameshachukua hatua mbalimbali ikiwa pamoja na kumuandikia Waziri mwenye kuhusika
na masuala ya ardhi kwa ufumbuzi wa suala hilo.
END.
Comments
Post a Comment