VIDEO-WAFANYABIASHARA SOKO LA MAILIMOJA WANATAKA SERIKALI KUWATHAMINI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/16/2016 8:42:21 AM
Wafanyabiashara
katika soko la Mailimoja halmashauri ya mji wa Kibaha wameitaka serikali
kuwalinda ili kuepuka changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji
wao wa majukumu yao ya kila siku.
Mratibu wa
wafanyabiashara nchini, BW.ALLY NDAUKA ameongea hayo katika mkutano wa
wafanyabiashara wa soko la Maili moja ambapo amesema wafanyabiashara wadogo
wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi.
BW.NDAUKA
ameongeza kuwa wafanyabiashara wamekuwa wakifilisiwa kutokana na uwepo wa
sheria stukizi ambazo mara nyingi huwasababishia wafanyabiashara hasara na hasa
ikizingatiwa wafanyabiashara hao wanaendesha biashara zao kwa mikopo.
Vox1-ALLY
NDAUKA
VOX
2-RAMADHAN NGOWO
Naye mmoja
wa wafanyabiashara sokoni hapo, BW.RAMADHAN NGOWO amepinga kufanyika kikao
hicho kutokana na kukosekana kwa Mkurugenzi wa mji na afisa biashara
wahalmashauri ya mji wa Kibaha.
Bw .NGOWO
amefafanua wamekuwa wakilipishwa ushuru mbalimbali kinyume cha taratibu kiasi
kwamba zinachangia kudumaa kwa biashara zilizopo ametoa mfano, ushuru wa
halmashauri ni shilingi 300 lakini wakusanya ushuru wanatoza shilingi 500, hali
ambayo inawaleta sintofahamu wafanyabiashara.
END.
Comments
Post a Comment