WAKAZI MKOA WA KAGERA KUFANYIWA UPASUAJI WA MDOMO SUNGURA BURE

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/7/2016 7:11:52 AM
Wananchi wa Mkoa wa Kagera kupitia taasisi isiyo ya kiserikali ya THE MIGHTY FORTERESS FOUNDATION ya Uholanzi wamebahatika kupata huduma ya upasuaji ya watu wenye matatizo ya mdomo sungura katika jitihada za kutoa huduma za afya kwa wahitaji.

Mwakilishi wa shirika hilo nchini, Mchungaji GERVAS MASANJA amesema wameamua kutoa huduma hiyo kutokana na kuwepo kwa wanajamii wenye tatizo hilo na kutoa fursa kwao kutumia nafasi hii adimu ya kupata upasuaji ambayo ingewagharimu fedha nyingi.

Mwakilishi huyo MCH.MASANJA amesema kwamba watashirikiana na wataalamu bingwa wa upasuaji kutoka nchini Holland wanaojulikana kama INTERPLAST HOLLAND pamoja na madaktari bingwa wa hapa nchini na zoezi hilo linatarajiwa kufanyika katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera  kati ya tarehe 26 machi mpaka tarehe 1 april , Machi 20 mpaka 25  upasuaji huo utafanyika katika hospitali ya Ndolage Bukoba.
END.


Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA