WANANCHI WATAKA HALMASHAURI IWAACHIE ENEO AMBALO WAMELIPIGANIA


Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/6/2016 10:36:21 AM
Umoja wa wakulima Soga umelalamikia hatua ya uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha kutumia nguvu kuwatoa eneo ambalo wao wamaeamua kulitumia baada ya kukaa muda mrefu na kugeuka shamba pori.

Wakizungumza na mwandishi wa Habari hizi, mmoja wa wakazi wa eneo hilo maarufu kama Kazamoyo, BW.MOHAMED CHETO amesema kuwa wao kama wananchi walianza harakati za kutaka kulitumia eneo hilo mara baada ya kuona ni muda mrefu limeachwa ilihali wao wana dhiki ya ardhi.

BW.CHETO amebainisha kuwa mara baada ya wao kuvamia ambaye anadaiwa kuwa mmiliki BW.JAHANGIR POPTAN alifungua kesi katika mahakama ya mwanzo Mailimoja akimshataki BW.YUSUPH KILIMA na wenzake 11, Ambapo hata hivyo mahakama hiyo ikaamuru akafungue kesi katika baraza la ardhi la wilaya na kuwaachia huru wote ambao walishtakiwa.

Lakini baada ya BW.JAHANGIR POPTAN kushindwa katika shauri hilo baadhi ya viongozi wa kijiji na Kata wamekuwa wakitumia nafasi zao kuwabugudhi wananchi kwa kutumia Jeshi la Polisi kuwafukuza, na wao wakiendelea kuuza kinyemela eneo hilo kwa maslahi binafsi.

Naye katibu wa umoja wa wakulima Soga, BW.OTHMAN RASHID amesema wao mpaka sasa wameshachukua hatua mbalimbali ikiwa pamoja na kumuandikia Waziri mwenye kuhusika na masuala ya ardhi kwa ufumbuzi wa suala hilo.


END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA