WANANCHI WAMTAKA MAKONDA AWASAIDIE BUNJU KITUNDA

Ben Komba/Kinondoni-Tanzania/3/8/2016 3:57:41 PM
Wakazi wa Bunju kwa Kidela ambao wanafikia kaya zaidi ya  hamsini wamemtaka Mkuu wa wilaya ya Kinondoni BW. PAUL MAKONDA kuingilia kati amri ambayo imetolewa na wakala wa majengo Tanzania kuwataka wahame eneo hilo mara moja.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo BIBI.GRACE SAGALA amesema yeye yupo hapo takriban miaka 10, lakini siku za hivi karibuni walikuwa wanashangaa kuona magari ya kiserikali yakifika hapo na kupimapima bila taarifa maalum.

BIBI.SAGALA amebainisha kuwa hali ilipofikia anaitaka serikali kuangalia suala hilo kwa undani ili kuwaepushia wananchi matatizo na wasiwasi ambao kwa njia moja au nyingine unaathiri ustawi wa afya ya jamii na hivyo amemuomba Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, BW.PAUL MAKONDA kuingilia kati.

Naye BW.DEOGRATIAS PETER amesema yeye ana takriban miaka 15 toka amehamia sehemu hiyo na hata siku moja hajawahi kupewa onyo lolote kutoka wizara ya ardhi.

Juhudi za kumpata Mtendaji mkuu wa TBA kwa njia ya simu hazikufanikiwa kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe wa simu ya mkono hakujibu.

Bw.PETER ameongeza kuwa yeye binafsi amefika mpaka wizarani kuulizia suala hilo ambalo Wakala wa majengo Tanzania (TBA) amelianzisha na kuwazushia hofu kubwa wananchi  ilihali wao wakiwa sio wamiliki wa eneo hilo.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA