VIDEO=ANATAFUTA NDUGUZE
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/17/2016 8:26:57 AM
Mwanamke
mwenye umri unaokadiriwa hamsini amewataka ndugu zake kujitokeza kumchukua
kutokana nay eye kuwa katika hali ya kutotambua anakoenda wala anakotoka.
Mwanamke
huyo ambaye amejitambulisha kwa jina la BI.ASIAT MASOUD amesema kuwa yeye
alikuwa ameolewa Jeshini Gongolamboto na kuishi katika kambi kama mmoja wa wake
wa wanajeshi wanaofanya kazi hapo.
Tatizo kubwa ambalo
analo BIBI.ASIAT MASOUD ni kuchanganya maneno unapojaribu kumhoji kujua
kulikoni juu ya maisha yake mpaka kujikuta akitangatanga katika mitaa ya mji wa
Kibaha.
Naye mmoja
wa wananchi ambao wamekuwa wakimsaidia huyo mama ambaye pia ni Mwenyekiti wa
soko la Mailimoja, BW. ALLY GONZI amewataka ndugu wa Mama huyu kujitokeza
kumchukua ndugu yao ili kumuepusha na dhiki anazokabiliana nazo
END.
Comments
Post a Comment