VIDEO - WAMTAKA DC MAKONDA AWASAIDIE
Ben
Komba/Kinondoni-Tanzania/3/8/2016 3:57:41 PM
Wakazi wa
Bunju kwa Kidela ambao wanafikia kaya zaidi ya
hamsini wamemtaka Mkuu wa wilaya ya Kinondoni BW. PAUL MAKONDA kuingilia
kati amri ambayo imetolewa na wakala wa majengo Tanzania kuwataka wahame eneo
hilo mara moja.
Mmoja wa
wakazi wa eneo hilo BIBI.GRACE SAGALA amesema yeye yupo hapo takriban miaka 10,
lakini siku za hivi karibuni walikuwa wanashangaa kuona magari ya kiserikali
yakifika hapo na kupimapima bila taarifa maalum.
BIBI.SAGALA
amebainisha kuwa hali ilipofikia anaitaka serikali kuangalia suala hilo kwa
undani ili kuwaepushia wananchi matatizo na wasiwasi ambao kwa njia moja au
nyingine unaathiri ustawi wa afya ya jamii na hivyo amemuomba Mkuu wa wilaya ya
Kinondoni, BW.PAUL MAKONDA kuingilia kati.
Naye
BW.DEOGRATIAS PETER amesema yeye ana takriban miaka 15 toka amehamia sehemu
hiyo na hata siku moja hajawahi kupewa onyo lolote kutoka wizara ya ardhi.
Juhudi za
kumpata Mtendaji mkuu wa TBA kwa njia ya simu hazikufanikiwa kufuatia simu yake
kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe wa simu ya mkono hakujibu.
Bw.PETER
ameongeza kuwa yeye binafsi amefika mpaka wizarani kuulizia suala hilo ambalo
Wakala wa majengo Tanzania (TBA) amelianzisha na kuwazushia hofu kubwa
wananchi ilihali wao wakiwa sio wamiliki
wa eneo hilo.
END
Comments
Post a Comment