VIONGOZI WANG'OLEWA BAGAMOYO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/1-1-2013 Wimbi la wananchi kung'oa viongozi wao kwa sababu mbalimbali limeshika kasi wilayani Bagamoyo na kwa wananchi kuchukua hatua ya kuwawajibisha viongozi wao kwa kukiuka taratibu za utumishi wa umma kwa kuweka mble maslahi binafsi badala ya wananchi kwa ujumla. Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia katika kipindi cha wiki moja wanachi wakichukua hatua ya makusudi ya kuwang'oa viongozi hao, wa Vijiji vya Ruvu Darajani na kijiji cha Milo vilivyopo katika Kata ya Vigwaza wilayani Bagamoyo katika mkoa wa Pwani mbele ya diwani wa kata ya Vigwaza, BW. MBEGU DILUNGA na mtendaji wa Kata BW. MASKUZI MASKUZI. Baadhi ya madai ambayo yamewagharimu uongozi katika vijiji vyote viwili ni matatizo ya uuzaji wa ardhi kiholela kinyume na taratibu za sheria, ambapo katika kijiji cha Ruvu Darajani wananchi waliujia juu wa uongozi kwa kutowashirikisha kikamilifu katika ugawaji wa maeneo na walipohojiwa katika kikao cha dharura cha kijiji hawakusema ukweli pamoja na wanachi kujua ukweli huo kitu ambacho kiliwakera wananchi. Mwenyekiti huyo wa kijiji cha Ruvu Darajani, BW. SALUM KWARO maarufu kama "Kambona" ambaye amevuliwa madaraka na nafasi yake kushikiliwa kwa muda na Mwalimu wa shule ya msingi Vigwaza, BI. MARY NZOWA,Mwenyekiti aliyeng'olewa BW. Kwaro alikuwa na wakati mgumu kuwasihi wananchi wamsikilize katika mkutano huo ili aweze kutoa ufafanuzi kuhusiana na eneo la soko ambalo ameligawa kwa kushirikiana na halmashauri ya kijiji kwa mtu binafsi bila kushirikisha wananchi jambo ambalo wananchi hawajakubaliana nalo. Aidha uongozi wa Mwenyekiti KWARO pia umedaiwa kuandika eka kidogo katika karatasi wanayoenda kuwasomea wananchi kwamba wamegawa kwa wawekezaji lakini ukifika eneo husika unakuta kubwa zaidi ilivyoandikwa, kitu ambacho wananchi wanaona kama kudanganywa na uongozi waliouchagua wenyewe na hivyo kuamua kuwavua madaraka viongozi wao. Mkazi wa Ruvu Darajani, BW. ATHUMAN GEREZA amesema uongozi umefanya sio, kwa kutoa eneo lao walilokuwa wanatumia kuuza mbogamboga kugawawiwa kinyemela kwa mwekezaji wasiyemfahamu na kuvunja banda lililokuwapo ikiwa pamoja na kuchukua bati zao bila kuwashirikisha wananchi wa Ruvu darajani kama sheria zinavyoelekeza. Mtendaji wa Kata ya Vigwaza, BW. MASKUZI MASKUZI amesema yeye kwa upande wake yupo pamoja na wananchi na hasa kutokana na kufuatilia mchakato na hoja zinazotolewa na pande zote mbili na kutoa mfano hapo Ruvu Darajani, ambapo tayari msingi umeshachimbwa katika eneo ambalo lilikuwa soko la mboga bila kuwashirikisha wananchi jambo ambalo halikubalikina hasa kutokana na wananchi kuamka na kutambua haki zao. END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA