WAZABUNI FEKIO CHANZO CHA KUZOROTA MAENDELEO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/01/01/2013/15:03:22 Kampuni iliyopewa zabuni ya kujenga matanki ya maji katika kijiji cha Milo kata ya Vigwaza wilayani Bagamoyo imewatelekeza wafanyakazi wake wake bila kuwapatia stahili zao na kuwafanya kuishi katika maisha ya mashaka hali ambayo inatishia ubora wa kazi wanayofanya. Mwandishi wa habari hizi akizungumza na wafanyakazi wa mzabuni huyo ambaye amepewa kazi ya kujenga matanki katika kijiji hicho, kupitia mradi wa maji unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wenye lengo la kusambaza maji maeneo ya vijijini ambapo kupitia fedha idara za maji za halmashauri wanasimamia utafutaji wa vyanzo vipya na maji na kusambaza.. Mwandishi ameshuhudia ujenzi wa kusuasua wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji katika kijiji cha Milo, hali inayosababishwa na mkandarasi kutokuwa makini katika utekelezaji wa shughuli hiyo ambayo imenuia kumaliza tatizo la maji katika kijiji hicho kilichopo umbali wa kilometa 25 kutoka barabara ya Morogoro. Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni huyo amemshauri mzabuni huyo kuachia kazi hiyo kutokana na kuonyesha kila dalili za kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi hiyo ipasavyo, na hasa ikizingatiwa sasa ni takribani miezi miwili na nusu na kazi ikiwa imefanyika kidogo tu, hivyo amewataka watumishi wa idara ya maji wilayani Bagamoyo kumfuatilia mkandarasi huyo kwa makini kutokana na kutotilia maanani kazi hiyo. Wafanyakazi hao wamefika mbali hata kutishia kuuza udongo ulaya mchache uliopo katika eneo hilo kutokana na mkandarasi huyo kununua vifaa kidogo kidogo, kwa upande wa wachimba mitaro nao hali kadhalika kwa upande mambo hayajatulia na huku Mlinzi aliye katika kijiji cha Kitonga akilalama kuhusu kutolipwa mshahara wake katika wakati. Kutokana na hali hiyo nilichukua hatua ya kumuona Diwani wa Kata ya Vigwaza, BW. MBEGU DILUNGA ameema kutokana na utaratibu uliowekwa na halmashauri kupitia vikao vya baraza la madiwani, kampuni ikishapewa zabuni inatakiwa iwe na fedha za kuanzia na kutokana na hilo mkandarasi huyo ameanza kazi hiyo kwa fedha zake mwenyewe mpaka kazi itakapokaguliwa ikifika hatua fulani ndipo aanze kulipwa. Hata hivyo ameaahidi kufuatilia suala hilo kujua iwapo mkandarasi huyo ameshalipwa ama hapana, ili kumuwezesha kuchukua hatua sahihi. Naye msimamizi wa kampuni hiyo niliyemfahamu kwa jina moja la PHILLIPO nilmtaka aeleze kwanini hali inakuwa hivyo amesema kuwa sio kweli kwamba kila mtu analipwa kwa kadri ya makubaliano, lakini kabla hajamaliza Mwenyekiti wa kijiji cha Kitonga aliwasili katika eneo hilo akiwa na malalamiko ya Mlinzi waliyemweka katika kijiji hicho kulinda pampu ya maji juu ya kutopata mshahara wake. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA