TRA na WALIPA KODI WAUNDA KAMATI YA PAMOJA PWANI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/21-Jan-13/15:53:58 Wadau wa kulipa kodi katika mkoa wa Pwani wamechagua kamati ya utendaji katika suala zima la ulipaji kodi kwa maendeleo ya nchi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia na kuratibu maazimio yote yanayofikiwa na kikao cha kila baada ya miezi mitatu chenye lengo la kutathimini masuala mbalimbali kati ya wadau na mamlaka ya kukusanya mapato {TRA}. Uchaguzi huo uliosimamiwa na Meneja wa TRA mkoa wa Pwani ambaye pia ni mwenyekiti wa kikao cha wadau, BIBI. HIGHNESS CHACKY, Ambapo Mwenyekiti wa kamati ya utendaji amekuwa BIBI. HIGHNESS CHACKY, makamu Mwenyekiti BIBI. KAASA MLONJA, katibu ni BW. BAKARI KAPERA, wakati wajumbe wengine wa kamati hiyo ya utendaji ya wadau wa kulipa kodi ni BW. SEHEL ABOUD, BW. WAKIL MURO, BW. ELISANTE NGURE, BW. LAMSON TULYANJE na BW. MAGARE MURYA. Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo wa kamati ya utendaji ya wadau wa kulipa kodi, Meneja wa TRA katika mkoa wa Pwani, BIBI. HIGHNESS CHACKY amesema katika mwongozo waliopewa ili kikao tunachokaa kikamilike ni lazima kuwepo kwa kamati ya utendaji ili kuweza kuleta tija kama ilivyotarajiwa kamati ya utendaji inawajibu wa kusimami sualka zima la ukusanyaji wa kodi katik ya wale wanaosimamia walipa kodi na walipa kodi wenyewe. BIBI. CHACKY amesema kamati hiyo itasimamia maazimio mbalimbali ambayo yatafikiwa katika kikao cha wadau wa kulipa kodi, masuala ambayo watahitaji kusimamiwa kwa undani ili kulinda haki katika pande zote mbili kati ya mkusanya kodi na mlipa kodi, kamati hiyo inamchanganyiko kutoka katika pande zote mbili. Amewataka wafanyabiashara kulipa kodi kwa serikali kutokana na kipato anachopata na amewashauri wafanyabiashara wanaoanzisha biashara mpya kutafuta ushauri kuhusiana na suala zima la kulipa kodi ili kuepukana na usumbufu usio wa lazima na kwa kulipa kodi ni njia ya kutimiza taratibu za kisheria za kuchangia sehemu ya kipato kama unazilisha milioni 4 kwa mwaka kwa ajili ya maendeleo ya taifa. Naye mmoja wa wawakilishi wa wafanyabiashara katika mji wa Kibaha, BW. ELISANTE NGURE amezungumzia matatizo yanayotokea katika mashine maalum inayotolewa na MAMLAKA YA MAPATO kwa ajili ya kukatia risiti wateja punde wanunuapo bidhaa ambayo upeleka taarifa moja kwa moja kwa mamlaka hiyo, ambapo wakati mwingine husumbua kutokana na kukosekana kwa mtandao na kuwapa wakati mgumu wafanyabiashara na hasa anapojitokeza mteja na mashine ya risiti imegoma. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA