WAKALIMANI WA LUGHA YA ALAMA WATAKA SERIKALI IWAAJIRI. Ben Komba/Pwani-Tanzania/27-Jan-13/17:31:20 Serikali nchini imetakiwa kuajiri wakalimani katika nyanja mbalimbali ikiwa sehemu ya kutambua uwepo wa walemavu wa kusikia, ambao kutkana na tatizo linalowakabili inakuwa ngumu kwao kupata taarifa juu ya maambo mbalimbali kutokana na kukosa nyenzo za kujimudu ikiwa pamoja na wakalimani. Mwandishi wa habari hizi nimebahatika kuzungumza na Mwanachama wa chama cha Tanzania Association of Sign Language Interpreters (TASLI), au chama cha wakalimani wa lugha ya alama Tanzania, BW. HABIB UPURUTE ambae amesema wamekuwa wakifanya kazi katika mazingiora magumu kutokana na watu wengi kufikiri kazi hiyo ni nyepesi, na hivyo kuifanya hata serikali kutotupia macho kada hiyo. BW. UPURUTE amebainisha walemavu wa kusikia wamekuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa kunakosababishwa na watu wengi katika jamii kutoifahamu barabara lugha ya alama na hivyo kuchangia kuwanyima fursa mbalimbali walemavu wenye matatizo ya kusikia akitoa mfano kama zoezi linaloendelea hivi sasa la mchakato wa kutengeneza katiba mpya ambapo wao kama walemavu wa kusikia wanashindwa kuyawasilisha maoni yao kutokana na kukosekana nyenzo za kujimudu. Akizungumzia juu ya matumizi ya lugha ya alama, BW. UPURUTE amebainisha kuwa lugha ya alama ni lugha kama lugha nyingine, ingawa nayo imegawanyika kulingana na lugha za kutamka zilivyo, lugha ya alama ya kimataifa inayotambulika ulimwenguni ni AMERICAN SIGNAL LANGUAGE (ASL), ambayo mlemaavu wa kusikia wa Afrika mashariki hawezi kuielewa isipokuwa kama amepata mafunzo ya lugha hiyo. Awali akifungua warsha hiyo kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa kusikia mjini Kibaha ambayo imeandaliwa na taasisi ya utafiti juu ya watu wasiosikia Tanzania (TADERE) mjini Kibaha, Diwani wa Kata ya Visiga, BW. OMARY NONGANONGA amewaasa walemavu nchini kushikamana na kuunda chombo kimoja ambacho kitawawakilisha katika kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili. Warsha hiyo imefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY. END.

Comments

  1. Picha ya juu kabisa ni mkalimani wa lugha ya alama kutoka TANZANIA ASSOCIATION OF SIGN LANGUAGE INTERPRETERS, BW. HABIB UPURITE akiwa kazini.Picha mbili nyingine ni baadhi ya washiriki wa warsha hiyto iliyofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro Park Misugusugu mjini Kibaha, Picha na Ben Komba.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA