MSURUR WA KODI WAWACHOSHA MAMA NTILIE.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-Jan-13/16:16:23
Wafanyabiashara katika kata ya Mailimoja wamelalamikia hatua ya ofisi ya kata ya kuwaambia kupima afya na kuwatoza fedha shilingi 5000/=, eti ikiwa ni ada ya upimaji kwa kila mfanyabiashara, jambo ambalo wamelipinga na kushangazwa na hatua hiyo.
Mmoja wa Kinamama mfanyabiashara wa chakula BI. FATUMA LAMBA amelalamika kuwa wamekuwa wakibugudhiwa na Bwana afya ya Kata na mgambo wake kwa kutumia muda mwingi kuwatishatisha wafanyabiashara hao ambao wanasema wanachokipta katika biashara hiyo ni kidogo, kulinganisha na halmashauri inavyowachukulia kama vile wanapata mafedha mengi.
Mfanyabiashara huyo ameshangazwa na kuzuka kwa msururu wa kodi ambao unamkandamiza mwananchi kisawasawa kiasi cha kuwafanya wananchi kuzua migomo ya hapa na pale, kutokana kujikuta wanawafanyia watu wengine kazi na kuwafaidisha huku familia zao zikiwategemea kwa hali na mali.
BI.LAMBA amefikia hatua ya hata kufikiria kuacha biashara hiyo kutokana na usumbufu wa mara kwa mara wanaoupata na hasa katikati ya mwezi inapotokea watu hawana fedha wao halmashauri wamekuwa wakiwazushia kodi mbalimbali kama ya uzoaji taka, mara pikipiki ili mradi mfanyabiashara mdogo hapumui.
Tukio hilo ambalo lilitokea majira ya saa nne usiku, na nilibahatika kuonana na Diwani Kata ya Maili Moja, BW. ANDREW LUGANO amesema Bwana afya wa Kata ameagiza kwa wafanyabiashara wa chakula katika eneo hilo la Mailimoja nyakati za jioni mpaka usiku wa manane kufika ofisini kwake na shilingi 5000/=, Ili wapatiwe fomu ya kwenda kupima afya.
BW. LUGANO kwa upande wake amesema yeye amewaambia wapiga kura wake kuwa anachofahamu ni kuwa kupima UKIMWI ni suala la hiari na hakuna gharama zozote zinazohitajika, Lakini kwa mujibu wa Bwana afya wa kata amesema suala hilo la upimaji wa UKIMWI kwa kutoza shilingi 5000/= ni la Taifa zima sio mjini Kibaha pekee yake.
END.
Comments
Post a Comment