KIBAHA TC YAPATA GREDA NA GARITAKA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/29-Jan-13/19:10:34 Halmashauri ya mji wa Kibaha imezindua Greda la kutengenezea barabara na gari la kubeba taka katika suala zima la uboreshaji wa usafi wa mazingira na uimarishaji w mipango miji kutokana na maeneo yote ambayo hayajapasuliwa barabara kutarajiwa kufikiwa. Akizungumza katika uzinduzi huo Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BI. LEAH LWANJI amebainisha kuwa gari la kubeba taka limetolewa na manispaa ya mji wa GOTLAND kwa ajili ya halmashauri ya mji mara baada ya ujumbe wa viongozi na madiwani kutembelea nchini SWEDEN na wenyeji wao kuwapatia zawadi ya gari hilo ili kusaidia kutunza mazingira ya mji wa Kibaha. BI. LWANJI amesema greda kwa ajili ya kuchonga barabara katika halmashauri ya mji na kukodisha hilo limepatikana kutokana mapato ya ndani ya halmashauri na limegharimu takriban shilingi milioni 528/= za kitanzania, akizungumzia juu ya vitendea kazi vingine kama gllovu, viatu na vinginevyo vimekuja pamoja na gari kwa ajili ya kutumiwa na watu ambao watahusika na uzoaji taka katika halmashauri ya mji wa Kibaha. Akiongea katika hafla hiyo mkuu wa wilaya ya Kibaha BIBI. HALIMA KIHEMBA kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Pwani, BIBI. MWANTUMU MAHIZA amesema wakazi wa Kibaha inawapasa kutambua kuwa sasa wanaishi mjini na kuanza kuachana na dhana ya kuchimba mashimo ya taka katika nyumba zao na kuanza utamaduni wa kukusanya taka hizo kwa ajili ya kwenda kutupwa katika eneo maalum. BIBI .KIHEMBA akizungumzia kuhusu Greda amesema ni hatua kubwa ambayo itasaidia kuimarisha barabara za halmashauri na kuwezesha kuboreka hali ya barabara katika mji huu. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA