UWT WAHIMIZWA UPENDO
UWT WAHIMIZWA UPENDO NA MSHIKAMANO.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/09-01-2013
Wanawake nchini wametakiwa washikamane kwa umoja wao kwani uchaguzi umeshakwisha na kilichobaki sasa ni kujenga chama kwa ajili ya kukiimarisha chama kuelekea chaguzi zijazo.
Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake Mkoa wa Pwani, BI. ZAINAB VULU katika baraza la mkoa la jumuiya hiyo, ambalo kati ya mambo mengine alisisitiza kuvunjwa kwa kambi.
BI.VULU amebainisha ili wanawake waweze kuyfikia malengo yao hawana budi kupendana, kushikamana iliu wakiwezeshe chama chao kufanya vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi kwa kuhakikisha maeneo yanayoshikiliwa na wapinzani yanarudi mikononi mwao.
Amefafanua kuwa katika kuhakikisha wanarejesha maeneo yanayoshikiliwa na wapinzani watahakikisha wanatekeleza ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni ya uchaguzi, ikiwa pamoja na kuwashughulikia watendaji ambao watakuwa hawatimizi majukumu yao ipasavyo.
Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya wanawake Mkoa wa Pwani, BI ZAINAB VULU amewaasa wanawake kujiingiza katika shughuli za uzalishaji mali ili kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa na SACCOS.
Amesema kwa upande wa jumuiya hiyo imejikita katika suala la VICOBA ili kutoa fursa kwa kinamama kujiwekea akiba na kupata uhalali wa kukopesheka kwa wale ambao wanafanya biashara za mbogamboga na za wastani ambao hawakopesheki kwenye mabenki.
END.
Comments
Post a Comment