SHERIA ZA KAZI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/14-Jan-13/18:59:14
Kukosekana kwa elimu juu ya sheria za kazi imesemekana ni kikwazo kikubwa kwa upatikanji wa haki sehemu za kazi kunakosababishwa kwa kiasi kikubwa wa uwepo wa vyama vya wafanyakazi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Msuluhishi mwandamiziwa tume ya utetezi na usuluhishi katika mkoa wa Pwani, BW. MWANGATA MAKAWA amesema viongozi wa vyama vya wafanyakai wanajua juu ya ukosefu wa elimu juu ya sheria za kazi kwa wanachama na waajiri.
BW, MAKAWA amebainisha kuwa ni wajibu wa Bwana kazi ambaye anapata wasaa kukagua maeneo ya kazi kumshauri mwajiri au mwajiriwa hatua za kuchukua anapoona haki yake inakiukwa, lakini ukosefu wa mafungu ya kuwezesha kutolewa elimu juu ya mfanyakazi, ndiyo kikwazo kikubwa kinachokwamisha uimarishaji wa haki za wafanyakazi.
Msuluhishi mwandamizi huyo wa tume ya usuluhishi na utetezi, BW. MAKAWA ameweka wazi kuwa utoaji wa mafunzo ni kitu muhimu kwani uzoefu unaonyesha sehemu ambazo zinatoa elimu juu ya sheria za kazi, uwa hazikumbwi na migogoro ya mara kwa mara kulinganisha na maeneo ambayo hayapati mafunzo hayo hivyo ametaka vyama vya wafanyakazi kutenga fedha kwa ajili ya kuwapatia wanachama elimu juu ya sheria za kazi.
BW. MAKAWA amekemea tabia ya baadhi ya waajiri kupuuza waitwapo katika mashauri juu ya migogoro ya kikazi inayojitokeza katika maeneo yao, na hivyo kusababisha kwa maamuzi kutolewa upande bila mwingine kuwepo mara baada ya kupewa wito wa kufika katika baraza hilo mara tatu kutokana na tume hiyo kutokuwa na watu wa kuwakilisha barua hizo kwa mwajiri na hivyo wakati mwingine zinaweza kuchelewa kumfikia mlengwa.
END.
Comments
Post a Comment