SACCOS YA WALIMU YASOTESHA WANACHAMA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/
Wanachama wa SACCOS ya walimu wilayanai Kibaha kwa takiban wiki mbili wamekuwa wakisotea mikopo kutoka katika SACCOS kwa ajili ya kutaka kutumia fedha hizo kwa matumizi mbalimbali bila mafanikio.
Mmoja wa walimu nilioongea naye ambaye hakupenda jina lake kuwa wazi, amesema wamekuwa wakifia katika Ofisi hizo za na kumbiwa bado hawajapata mrejesho kutoka halmashauri na hasa kutokana na fedha hizo kukata moja kwa moja katika mshahara.
Mwalimu huyo anashangazwa kwa nini kuwepo na mizunguko ili hali wanachama wamekuwa wanaweka akiba kama wanavyostahili iweje leo wanahitaji kuchukua fedha za kwa ajili ya kutumia kwa ajili ya maandalizi ya watoto shule wanazikosa katika wakati na kuambulia kuzungushwa hali ambayo inawatia wasiwasi iwapo akiba zao zipo katika mikono salama.
Mwalimu mwingine naye ameongeza yeye amesikia kuwa halmashauri ya mji imeshatoa fedha shilingi milioni 11 kwa SACCOS hiyo ikiwa marejesho ya makato yaliyofanywa na halmashauri kutokana na makato ya katika mshahara na halmashauri ya wilaya ya Kibaha yenyewe nayo imetoa marejesho ya shilingi Milioni 8 ili kuwezesha walimu kukopeshwa fedha wanazohitaji.
Mwanachama huyo ameongeza kuwa SACCOS hiyo imekuwa mkama wakala wa Benki kutokana na kutokuwa na uwezo wa kukopesha na 9inatumia kanuni za kibenki katika kuwakopesha wanachama wake na kuziweka kando zile za vyama vya ushirika.
Mwenyekiti wa SACCOS hiyo aliyejulikana kwa jina moja tu, La MWL. MANYAKALA amewalaumu wananchama wake kwa kuwa wepesi wa kuwapeleka Polisi viongozi wao, bil kutoa nafasi ya kuwasiliza viongozi wao, ili kupata ufafanuzi juu ya kitu gani hasa kinajiri katika ushirika wao huo wa kuweka na kukopa.
SACCOS ya chama cha Walimu Kibaha ina wanachama 4000 ambao wengi wao ni walimu, na kinakusanya takribani shilingi milioni 19 kwa mwezi kutoka kwa wanachama wake.
END.
Comments
Post a Comment