BARAZA LA BIASHARA LAZINDULIWA KIBAHA.
BARAZA LA BIASHARA LAZINDULIWA KIBAHA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/
Halmashauri ya wilaya ya Kibaha imezindua rasmi baraza la biashara katika kuweesha majadiliano na mijadala ya mashauriano ya mara kwa mara kwa watu binafsi na serikali ikiwa pamoja na kuboresha mazingira ya shughuli wanazofanya.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BIBI. TATU SELEMANI amesema kuwa Baraza hilo litajumisha sekta binafsi, Asasi zisizokuwa za kiserikali na sekta za umma wale wote wanaohusika na utoaji wa huduma kwa jamii.
BIBI. SELEMANIameongeza hatua hiyo kuonyesha kuwa serikali inatambua kuwa changamoto ya kuleta maendeleo ya nchi haiwezi kuachiwa sekta moja, bali malengo yanaweza kufikiwa kwa sekta hizo kila mmoja ikimuweesha mwenzake, na ametaja kuwa ni ubia ambao ni mfumo sahihi wa kufikia malengo ya Taifa ya kutoa huduma ya kukidhi mahitaji ya jamii ambayo yasingeweza kufikiwa pasipo nguvu ya pamoja.
Awali akisoma taarifa ya kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Pwani, BIBI. MWANTUMU MAHIZA, Mkuu wa wiulaya ya Kibaha, BIBI HALIMA KIHEMBA amesema pamoja na kuchelewa kuzinduliwa mapema kwa baraza hilo katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha inatakiwa kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha linasimama na pande zot husika kuwa tayari kuchangia.
BIBI. KIHEMBA amefafanua dhima nzima ya kuanzisha baraza la biashara la Taifa ilikuwa ni kutoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza na kuzalisha ajira mpya na hasa kuzingatia mchango mkubwa unaotolewa na sekta binafsi katika maendeleo ya Taifa na kutoa mfano wa ujenzi wa mahoteli unaoendelea kwa sasa nchi nzima, amebainisha kuwa ni kukua kwa uwekezaji nchini.
Uamuzi wa kuunda mabaraza ya biashara ya mikoa na wilaya nchi nzima uliafikiwa 15 Machi, 2005 wakati wa mkutano wa tatu wa Barza la Taifa la Biashara na uzinduzi wa mabaraza ya wilaya ulifanywa na Rais JAKAYA KIKWETE tarehe 04 Desemba 2008.
END.
Comments
Post a Comment