POLICE FAMILY DAY NA SHERIA KANDAMIZI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/17-Jan-13/14:04:59
Katika siku ya kuadhimisha POLICE FAMILY, Jeshi la Polisi katika mkoa wa Pwani limefanya maandamano ya amani ambayo yaliishia katika kituo cha afya Mkoani katika halmashauri ya mji wa Kibaha na kufanya shughuli za usafi katika maeneo ya kituo cha afya.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Pwani, Kamishna msaidizi wa Polisi ULRICH MATEI akizungumza katika maadhimisho hayo amesemaleo ndio siku ambayo Jeshi la Polisi katika mkoa wa Pwani linaadhimisha siku ya Familia na Polisi na kati ya mambo ambayo walipanga kuyafanya ni kufanya usafi maeneo ya kituo cha afya Mkoani ikiwa pamoja na kujadili changamoto na mafanikio ya kiutendaji waliyoyakabili katika mwaka 2012.
Ambapo Kamishna msaidizi MATEI amebainisha kuwa mkoa wa Pwani umeonyesha kupata mafanikio ya kuridhisha katika nyanja ya kiuslama ingawa palikuwa na matishio kadhaa ambayo yaliweza kutokea katika nyakati tofauti, akatoa vurugu kati ya wakulima na wafugaji wilayani Rufiji ambazo zilisababisha hasara kubwa kwa jamii na Jeshi la Polisi
Ameongeza kuwa mikakati ya kuzuia uhalifu katika mkoa wa Pwani ni endelevu na shirikishi ambapo Jeshi la Polisi katika mkoa wa Pwani limeendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kuzuia kutanzua kero ya uhalifu katika maeneo yao, aidha amezungumzia juu ya jitihada zinazofanywa na Jeshi hilo katika kuzuia vurugu za kidini ambapo Jeshi hilo mkoani hapa limeshachukua hatua kwa kukaa na viongozi wa dini kuhakikisha vurugu hizo haziaamii mkoa wa Pwani.
Naye katibu tawala wa wilaya Kibaha, BW. JUSSEIM MWAKIPESILE akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Kibaha, BIBI. HALIMA KIHEMBA amesema Jeshi mla Polisi katika kufanya usafi katika kituo cha afya Mkoani wameonyesha ushiriki wao katika masuala ya kijamii na kunogeza dhana nzima ya Polisi shirikishi jamii na kutambua kwenu umuhimu wa kulinda afya kwani Polisi Mgonjwa hawezi kulinda Taifa lake.
Hivyo amewaomba kuzingatia umuhimu wa kutnza afya hasa katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya maambukizi ya HIV/AIDS na maradhi mengine kama vile malaria na homa ya matumbo ili kulinda nguvu kazi ya Taifa.
END.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/Wednesday, January 16, 2013/20:07:27
Wananchi mjini Kibaha wamelalamikia hatua ya halmashauri ya mji wa Kibaha kuanzisha sheria ndogondogo zinazowaathiri kiuchumi kutokana na nyingi za sheria hizo kuwa kandamizi kwa kuwaadhibu wananchi kwa faini kubwa ambazo zimekosa makadirio sahihi.
Nikiongea na Mama mmoja mfanyabiashara ambaye hakutakutaka kutaja jina lake, amesema mgambo hao wanaotumika kuwakamata watu wamefikia hatua ya kuzuia wafanyabiashara kupanga bidhaa zao wanazoziweka mbele ya maduka yao kwa kisingizio kuwa ni takataka na hivyo kuwaweka katika wakati mgumu.
Mfanyabiashara huyo ameelezea kushangazwa kwake na usafi huo unaofanywa na halmashauri ya mji toka hakuna vizimba vya kutosha vya kuhifadhia taka na matokeo yake takataka zinazokusanywa zinaende kutupwa eneo ambalo sistahili kutokana na kuwepo karibu na makazi ya watu na karibu mita 20 kutoka ofisi ya Kata ambalo wakati mwingi kutokana na mrundiko wa takataka eneo hilo hutoa harufu kali.
Mbali ya hayo Mfanyabiashara huo ameshangazwa na hao watu wanaosimamia suala usafi wa mazingira mjini Kibaha kwa kutoitupia macho ofisi ya Kata yenyewe ambayo imekosa choo kwa ajili mya watu wanaofika kupata huduma ofisini hapo, eneo ambalo hata Bwana afya wa Kata ana ofisi, na kuita kinachofanyika kama ukandamizaji wa wananchi.
Naye Kijana mjasiriamali wa Maili moja yeye amesema hali ni mbaya majumbani kutokana na watu hao wanaoambatana na mgambo, kulazimisha wananchi katika kila chumba kulipia shilingi 700/= ili taka zao zizolewe ikiwa sawa na kuwapiga marufuku wananchi kutafuata njia zao wenyewe za kuhifadhi taka hizo bila kuleta athari.
Kijana huyo amemtaja kada mmoja wa Chama Cha Mapinduzi ndiye anayeongoza harakati hizo, na kuita kitendo hicho ni cha kibepari na kinadhulumu haki za wananchi kwa kuanisha sheria ndogondogo mbalimbali ambazo zinakuwa na athari kwa mwananchi kiuchumi, ameomba wizara ya serikali za mitaa kuangalia kodi ndogondogo zinazotungwa na halmashauri kwani nyingi ni kandamizi.
Naye Bwana afya wa Kata ya Maili moja, BW. ALLY BAKAR SHAH ameendelea kusisitioza suala la usafi ni suala ambalo lipo siku nyingi na kila mmoja analitambua na elimu imekuwa inatolewa kwa wananchi ili waweze kuelewa lengo hasa la utaratibu huo mpya ambao amewahakikishia wananchi utaendelea kuwepo toka hizo ni sheria ndogo za halmashauri, aidhaBW. SHAH amekanusha kutokuwepo kwa choo katika ofisi ya Kata ya Maili moja.
END
Comments
Post a Comment