MGANGA AFUNGA KITUO AWAACHA HOI WANANCHI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/01-Jan-13/15:42:58
Katika hali ya kushagngaza katika kijiji cha Milo kata ya Vigwaza wilayani Bagamoyo, mganga wa kituo cha afya kijijini hapo amefunga kituo na kuondoka na funguo kwa kile ambacho amedai kufuatilia mafao yake na kuacha wananchi bila huduma hiyo muhimu.
Daktari huyo BW. ELIAS FELICIAN ambaye alikuwa akisaidiwa na wahudumu wawili wa kijiji hicho, BW. MICHAEL MAJALIWA na mwenzie BI. ASHURA MWINYI, wamebaki wamepigwa butwaa baada ya Mganga huyo wa kituo kufunga kituo hicho cha afya na kuondoka na funguo tofauti na alivyokuwa akifanya awali ambapo walikuwa wanaachiwa funguo na kuendelea kutoa huduma hiyo muhimu.
Mmoja wa Wahudumu hao, BW. MICHAEL MAJALIWA amebainisha wao walichaguliwa na mkutano mkuu wa kijiji kuwa wahudumu wa afya ya msingi kijiji hapo, na wamekuwa wakilipwa shilingi 15000/= kwa mwezi katika nyakati za mwanzo, lakini kila muda ulivyokuwa unasonga mbele, wakawa hawapati stahili zao kutoka serikali ya kijiji lakini kwa sasa wana miezi 13 hawajalipwa posho hiyo.
Mkazi wa kijiji hicho, BW. THOMAS DAREBA amesema yeye anashangazwa na hatua ya mganga huyo wa zahanati ya Milo kuamua kufunga kituo na kuondoka na funguo kana kweamba wananchi hawataugua tena hali ambyo inawanyima raha na hasa ikizingatiwa umbali uliopo kutoka kijijini hapo mpaka inapotolewa huduma hiyo ya afya.
Naye Mjumbe wa kamati ya afya ya kijiji hicho BW. JOHN MANGUNGU aemesema utokaji wa mganga huyo wa kituo hakupata taarifa yoyote rasmi, lakini kutokana na kusikia hivyo alikwenda kituoni hapo kushuhudia mwenyewe iwapo kama kweli kituo hicho kimefungwa na alikuta hali hiyo na kuamua kuondoka bila kujua hatima ya mganga huyo.
BW. MANGUNGU ameiomba halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kupeleka mganga mwingine kutokona na aliyekuwepo awali kuondoka kwani huduma ya afya ni kitu cha msingi kwa ajili ya ujenzi Taifa lenye watu wenye afya bora.
END.
END
Comments
Post a Comment