TANESCO YANUIA KUIMARISHA UTOAJI HUDUMA PWANI.

TANESCO PWANI YAJIPANGA KUBORESHA HUDUMA. Ben Komba/Pwani-Tanzania/30-Jan-13/08:23:59 Shirika la umeme katika mkoa wa Pwani linatarajia kufikia wateja elfu 17500 kwenye kipindi cha mwaka 2013-2014 ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wanafiki wateja wengi zaidi katika lengo la kuwafikia wateja 250,000 nchi nzima sawa na kupunguza bei ya uunganishaji wa huduma hiyo kwa wateja. ... Meneja wa TANESCO mkoa wa Pwani, BW. JOHNSON MWIGUNE amesema shirika hilo lina mikakati ya kurekebisha utoaji huduma, kwa kuhakikisha kuna kuwa na ongezeko la wateja wapya ili kuongeza makusanyo ya kila mwezi ya shirika, na katika kuvutia wateja shirika limeanza kwa kushusha bei ya kuunganisha huduma hiyo kwa wateja wa kawaida hali ambayo inatoa fursa kwa watu wenye kipato cha kati kupata huduma hiyo. BW.MWIGUNE amesisitiza kuwa shirika lake litaendelea na zoezi la ufungaji wa mita za luku kwa wateja wake katika suala zima la matumizi ya digitali na kuachana na Mita za analogia na zoezi hilo limefanikiwa kwa asilimia 95 mpaka sasa na wateja wengi wameonyesha kuifurahia huduma hiyo kutokana na mteja kuwa na mamalaka kamili ya kuamua muda ambao atahitaji huduma kulingana na kipato chake. Meneja huyo wa TANESCO katika mkoa wa Pwani, BW. JOHSON MWIGUNE ameongeza kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali likiwamo suala la wizi wa mafuta ya Transfoma ambalo kwa sasa shirika limefanikiwa kulidhibiti kutokana na uwepo wa ulinzi shirikishi na kuletwa kwa kwa matransfoma yanayotumia seli kavu badala ya mafuta, na kutokana na hilo shirika limeelekeza nguvu zake katika kubadilisha Tranfoma kutoka za mafuta kwenda kwa transfoma za seli kavu. Aidha amewataka wateja ambao wanadaiwa na shirika hilo na wamekatiwa kupata huduma hiyo, kufika ofisi kwao ili watumie fursa iliyotolewa na shirika hilo katika kipindi cha mwezi Januari mpaka June ya kuondolewa riba ya madeni yao kwa kuwekeana mkataba na wateja wanaodaiwa na kuwarudishia umeme huku wakiwajibika kulipa deni lao kidogo kidogo. BW. MWIGUNE ameweka wazi nia ya shirika kuwashawishi wadeni wakubwa kulipa madeni yao ili kuwezesha shirika kutekeleza malengo iliyojiwekea katika kuhkikisha wana boresha mazingira ya utoaji wa huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya Taifa. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA