VIDEO-WAUUGUZI WAPONGEZWA KWA KUJITOA KUSAIDIA WAGONJWA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/13/05/2016 11:34:06
Wauguzi nchini wamepongezwa kutokana na mchango wao wanaoutoa kwa binadamu wenzao wanapokabiliwa na magonjwa mbalimbali.

Mbunge wa Kibaha mjini, Mh. SLYVESTER KOKA amesema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani ambayo yamefanyika katika Hospitali teule ya rufaa ya Mkoa ya Tumbi.

Ambapo amesema muuguzi hana tofauti na Mama linapokuja kwenye suala la malezi ya mgonjwa, ametoa mfano  mtoto anapokuwa amejichafua aidha kwa kujikojolea au kujinyea ni aghalabu Baba kumchukua na kumbeba mpaka pale mama atakapomsafisha.

Mbunge huyo BW. KOKA amefananisha hali hiyo na mgonjwa anapokuwa hawezi kufanya lolote na kujisaidia mahali halipo ni muuguzi ndiye anayekuwa karibu naye bila kujali kama ni ndugu au la.

Naye Kaimu muuguzi mkuu wa Hospital ya Tumbi, BW. DAVID WAWA amesema kuwa siku ya wauguzi duniani ni maalum kwa ajili ya kukumbushana wajibu wao ikiwa pamoja na kula kiapo kipya ili kusaidia kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Aidha Kaimu muuguzi  mkuu huyo amemshukuru Mbunge huyo wa Kibaha mjini, BW.SYLVESTER KOKA kwa mchango wake wa shilingi milioni mbili kwa wauguzi ili ziweze kuwasaidia katika changamoto mbalimbali zinazowakabili.


END. 

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA