VIDEO-MAANDAMANO YA WAFANYABIASHARA KIBAHA YAZUIWA NA POLISI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/26/05/2016 14:34:40
Maandamano
ya wafanyabiashara wa soko la Maili moja mjini Kibaha kulalamikia hatua ya
halmashauri ya mji kutowajengea soko na ilihali wakitakiwa kuhama eneo ambalo
kwa hivi sasa linatumika kabla zoezi la bomoaaboma halijaanza yamenyimwa kibali
na Jeshi la Polisi.
Maandamano
hayo ambayo yangehusisha wafanyabiashara wa soko hilo yalipangwa kuelekea moja
kwa moja katika ofisi za Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha,
kutokana na kutaka kuonana naye kwa kipindi kirefu bila mafanikio.
Kwa mujibu
wa Katibu wa umoja wa wafanyabiashara sokoni Mailimoja, BW. MUHSIN ABDUL
amewaambia wafanyabiashara waliokusanyika sokoni hapo kuwa maandamano ambayo
walikuwa wayafanye yamesitishwa na Jeshi la Polisi kutokana na kuhofia uvunjifu
wa amani ambao ungeweza kujitokeza.
Naye
Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara hao, BW. ALLY GONZA maarufu kama Mzee wa
Shamba, amewataka wafanyabiashara kuwa watulivu kungojea hatua nyingine ambazo
watazichukua kabla ya zoezi la ubomoaji halijaanza.
VOX 1-
MWENYEKITI ALLY GONZA
VOX 2-VOX
POPULI
BW. GONZA
ameongeza kuwa Kibaha hakuna machimbo ya madini wala kitu chochote, hivyo
wafanyabiashara wameingiwa na hofu ya kutetereka kimitaji iwapo sula la
uhamishaji wa soko halitafanywa kwa umakini na kuongeza kundi la watu wasio na
kazi nchini.
END
Comments
Post a Comment