VIDEO-KIKONGO WILAYA YA KIBAHA WALALAMIKIA HALMASHAURI KUHUJUMU MAPATO YAO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/21/05/2016 10:43:00
Wananchi wa
Kata ya Kikongo wamelalamikia halmashauri ya wilaya ya Kibaha kusitisha
uchimbaji wa madini ya mchanga ambao ulikuwa unaipatia Kata hiyo mapato na
kutoa fursa hiyo kwa mtu binafsi.
Mwenyekiti
wa zamani wa serikali ya kijii cha Kikongo, BW. JUMA JUYA amesema kuwa akiwa
katika hiyo amesema akiwa mkusanyaji wa
fedha za mchanga ikiwa pamoja na
kuwasomea mapato na matumizi na wakawa wanaenda sawa na wananchi.
BW.JUYA
ameongeza makusanyo ambayo yalikuwa yanapatikana yalitumika katika shughuli
mbambali za maendeleo ikiwa pamoja na kutoa ajira kwa vijana zaidi ya hamsini
ambao waliweza kujikimu kimaisha.
Naye BW.
SALUM SAID amesema kuwa wamestuka kwamba mapato ya kijiji ya yanahujumiwa
kutokana na wananchi kuamua kuunda kamati ya muda ya kusimamia shimo hilo
ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja wa kamati ya muda iliweza kukusanya
takriban shilingi milioni 3.5 na hivyo kuweka wazi mapato ambayo yalikuwa
yanaishia mifukoni mwa wachache.
Baada ya
halmashauri ya Kibaha kuona wananchi wamechukua hatua ya kusimamia machimbo yao
wenyewe waliamua kusimamisha uchimbaji wa mchanga na kumtafuta mkandarasi
binafsi wa kuchimba mchanga huo na kukiacha kijiji hakina mapato.
BW. SAID
ameitaka TAMISEMI kuainisha vyanzo vya mapato vya halamshauri na vyanzo vya
mapato ya kijiji ili kuepusha mkanganyiko ambao unalenga katika maslahi binafsi
zaidi.
Juhudi za
kuonana na viongozi wa halmashauri ya wilaya Kibaha ili kutoa ufafanuzi
ziligongwa mwamba ikiwa pamoja na kuwasiliana nao kwa simu na Afisa mazingira,
BIBI ANNA MULEBA na Mkurugenzi TATU SELEMAN ambao muda wote hawakutoa
ushirikiano stahili.
END.
Comments
Post a Comment