UVCCM KIBAHA MJINI YAHIMIZA UTALII WA NDANI


Ben Komba/Pwani/Tanzania/12/05/2016 10:49:28
Katika kuhamasisha utalii wa ndani umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi hivi karibuni kimefanya ziara katika mbuga za wanyama  Mikumi ili kuunga mkono mkakati wa serikali katika kuwahamasisha wazawa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ambaye aliambatana na msafara huo, Mwenyekiti wa UVCCM mjini Kibaha, BW. IDD KANYALU amesema lengo kubwa la ziara hiyo ni kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali katika kuhamasisha utalii ndani na kuongeza kipato kwa Taifa.

BW.KANYALU amebainisha mbali ya lengo kuu hilo pia ni pamoja na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama na viongozi wa umoja wa vijana wa CCM mjini Kibaha kwa kuwawezesha kuwaweka pamoja na kutafakari mambo mbalimbali yta kukimarisha chama.

Mhifadhi wa Mbuga ya wanyama wa Mikumi BW. ABDALLAH CHOMA amewaambia watalii hao wa ndani kuwa wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha mbuga hiyo inabaki katika ubora wake.

Na akawatahadharisha watalii hao wa ndani kuwa watulivu kipindi chote watakachokuwa ndani ya mbuga ikiwa pamoja na kutotupa taka hovyo.


END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA