VIDEO-UTALII WA NDANI WAHIMIZWA
Ben
Komba/Pwani/Tanzania/12/05/2016 10:49:28
Katika
kuhamasisha utalii wa ndani umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi hivi
karibuni kimefanya ziara katika mbuga za wanyama Mikumi ili kuunga mkono mkakati wa serikali
katika kuwahamasisha wazawa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo
nchini.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi ambaye aliambatana na msafara huo, Mwenyekiti wa
UVCCM mjini Kibaha, BW. IDD KANYALU amesema lengo kubwa la ziara hiyo ni kuunga
mkono kwa vitendo juhudi za serikali katika kuhamasisha utalii ndani na
kuongeza kipato kwa Taifa.
BW.KANYALU
amebainisha mbali ya lengo kuu hilo pia ni pamoja na kujenga umoja na
mshikamano miongoni mwa wanachama na viongozi wa umoja wa vijana wa CCM mjini
Kibaha kwa kuwawezesha kuwaweka pamoja na kutafakari mambo mbalimbali yta
kukimarisha chama.
Mhifadhi wa
Mbuga ya wanyama wa Mikumi BW. ABDALLAH CHOMA amewaambia watalii hao wa ndani
kuwa wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha mbuga hiyo inabaki
katika ubora wake.
Na
akawatahadharisha watalii hao wa ndani kuwa watulivu kipindi chote
watakachokuwa ndani ya mbuga ikiwa pamoja na kutotupa taka hovyo.
END
Comments
Post a Comment