MAHAKAMA YALALAMIKIWA KUPOTOSHA HUKUMU
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/08/05/2016 14:49:31
Katika hali
ya kushangaza mahakama ya wilaya ya Kisarawe imemuhukumu kifungo cha mwaka
mmoja cha nje, Mtuhumiwa PETRO GEMBE kwa kosa la uvamizi na ubakaji iliyokuwa
inamkabili akishtakiwa na Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa nakala ya hukumu ambayo
mwandishi wa habari hizi ameipata, Inadaiwa tarehe 24 Juni mwaka 2015
mtuhumiwaPETRO GEMBE akiambatana na wenzie majira ya saa moja usiku walivamia
makazi ya BW.FESTO LOYA kwa nia ovu.
Inasemekana
mtuhumiwa huyo na wenzie walipora mifugo ng”ombe 53 na wenye thamani
21,000,000/= na fedha taslimu shilingi
milioni 48,350,000/= ambapo vitu vyote vilivyoporwa vina thamani ya shilingi
milioni 69,350,000/= mali ya BW. FESTO
LOYA ikiwa pamoja na kuondoka na mkewe DANGA’U GEIDA na kuishi naye kama mke
bila idhini yake.
BW.LOYA
amebainisha akiwa mkazi wa kijiji cha Kimalamisale amesikitishwa na hukumu hiyo
iliyotolewa na hakimu mkazi wa mahakama
ya wilaya ya Kisarawe BW. HAMIS SALUM kwa sababu haki haijatendeka kwani kosa
la uvamizi ,uporaji na ubakaji wa Mkewe hakiwezi kulingana na hukumu ya kifungo
cha nje mwaka mmoja.
Na ameitaka
mahakama kutoa haki na sio kuuza haki kama ilivyojidhirisha katika kesi hiyo,
kwani kwa kufanya hivyo baadhi ya wananchi wam ekuwa wakipoteza haki zao
kutokana tu na umaskini hata kama wakiwa wao ndio wana haki.
END
Comments
Post a Comment