VIDEO-WAJAWAZITO WASAIDIWA MJINI KIBAHA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/28/05/2016 13:40:29
Taasisi ya
Kimataifa ya Uingereza ya hiyari ya ABUBAKAR DARWESH imetoa msaada kwa akinamama
wajawazito wa Kituo cha afya mkoani Mjini Kibaha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji
wa utaratibu ambao wamejiwekea katika kusaidia jamii zenye mahitaji.
Mkurugenzi
wa taasisi hiyo BW. BILAL DARWESH akikabidhi msaada bhuo amesema kuwa amevutika
kutoa misaada ya kiutu kufuatia safari ambayo amefanya toka Dar es Saalam mpaka
Sumbawanga na kushuhudia changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi.
Msaada ambao
umetolewa na taasisi hiyo ni mabeseni na kila hitaji la mtoto anapozaliwa
vikiwa vimefungwa kwa pamoja, aidha ameongeza kuwa Taasisi yake
inajishughulisha na usaidizi kwa watu wa imani zote na ikiwa ni moja la lengo
kubwa la uanzishaji wake ili kuwawezesha watu wa imani tofauti kuishi pamoja.
Naye mganga
mkuu wa halmashauri ya mji wa Kibaha, DR. HAPPINESS NDOSI ameishukuru taasisi
hiyo kwa msaada ambao wameutoa kwa kina mama wajawazito ikiwa imeenda sambamba
na juhudi za serikali ya kupunguza vifo vya mama na mtoto kabla na baada ya
kujifungua.
DR.NDOSI
amechukua fursa kuelezea changamoto mbalimbali zinazokikabili Kituo cha afya
Mkoani, ikiwa pamoja na mahitaji makubwa ya chumba cha upasuaji.
Mama
mjamzito MARIAM ALLY yeye ameelezea uchache wa vitanda ambao unawalazimisha
kulala wawili na hivyo kuwalazimu kinamama kulala chini kuwapisha watoto
wanapozaliwa.
Na ameiomba
serikali kutatua tatizo hilo ili kufikia malengo ya kupunguza vifo vya
mama mtoto kabla na baada ya kujifungua.
END.
Comments
Post a Comment