WANANCHI WA KATA PANGANI MJINI KIBAHA WASAKA DARAJA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/21/05/2016 12:15:47
Wakazi wa
mtaa wa Mkombozi katika halmashauri ya mji wa Kibaha wameazimia kujenga daraja
litakalounganisha manispaa ya Kinondoni na halmashauri ya mji wa Kibaha ili
kupunguza usumbufu unaowapata wananchi wa pande hizo wakati wa mvua.
mmoja wa
wakazi wa Mtaa huo ambaye hakupenda kutajwa jina lake amesema kuwa wao kama
kamati ya ujenzi wa daraja hilo walikagua maeneo yote ambayo wanadhani panafaa
kujenga daraja.
Ambapo hapo
palizuka vuta nkuvute kati ya wajumbe wa kamati hiyo na kila mmoja akipenda
eneo tofauti kwa ajili ya ujenzi huo na katika kipindi hicho tayari fedha zaidi
ya shilingi milioni mmoja zilikuwa zimeshakusanywa.
Walikatishwa
tamaa na kauli ya mmoja wa wataalamu wa ujenzi kutoka halmashauri ya mji wa
Kibaha ambaye aliwaambia kujenga daraja eneo hilo kungehitaji zaidi ya shilingi
bilioni ambapo katika kipindi hicho
hawakuwa nazo fedha hizo.
Diwani wa
Kata ya Pangani, BW.AGUSTINO MDACHI amewataka wananchi kusahau yaliyopita ili
waanze kuanza upya mkakati wa ujenzi wa daraja hilo lenye manufaa ya kiuchumi
na kijamii kwa jamii ya Kata ya Pangani.
BW, MDACHI
amebainisha Kata ya Pangani imekuwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali
kunakosababishwa na uwepo wake pembezoni mwa mji wa Kibahai ikiwemo ukosefu wa
soko, huduma za afya na huduma nyingine muhimu kutokana na umbali kutoka Kata
hiyo kwenda Kibaha na kulinganisha na ukaribu wa kwenda manispaa ya Kinondoni.
END
Comments
Post a Comment