POLISI YAZUIA MAANDAMANO YA WAFANYABIASHARA


Ben Komba/Pwani-Tanzania/26/05/2016 14:34:40
Maandamano ya wafanyabiashara wa soko la Maili moja mjini Kibaha kulalamikia hatua ya halmashauri ya mji kutowajengea soko na ilihali wakitakiwa kuhama eneo ambalo kwa hivi sasa linatumika kabla zoezi la bomoaaboma halijaanza yamenyimwa kibali na Jeshi la Polisi.

Maandamano hayo ambayo yangehusisha wafanyabiashara wa soko hilo yalipangwa kuelekea moja kwa moja katika ofisi za Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha, kutokana na kutaka kuonana naye kwa kipindi kirefu bila mafanikio.

Kwa mujibu wa Katibu wa umoja wa wafanyabiashara sokoni Mailimoja, BW. MUHSIN ABDUL amewaambia wafanyabiashara waliokusanyika sokoni hapo kuwa maandamano ambayo walikuwa wayafanye yamesitishwa na Jeshi la Polisi kutokana na kuhofia uvunjifu wa amani ambao ungeweza kujitokeza.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara hao, BW. ALLY GONZA maarufu kama Mzee wa Shamba, amewataka wafanyabiashara kuwa watulivu kungojea hatua nyingine ambazo watazichukua kabla ya zoezi la ubomoaji halijaanza.

BW. GONZA ameongeza kuwa Kibaha hakuna machimbo ya madini wala kitu chochote, hivyo wafanyabiashara wameingiwa na hofu ya kutetereka kimitaji iwapo sula la uhamishaji wa soko halitafanywa kwa umakini na kuongeza kundi la watu wasio na kazi nchini.


END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA