VIDEO-MAHAKAMA YALALAMIKIWA KUPOTOSHA HUKUMU KISARAWE


Ben Komba/Pwani-Tanzania/08/05/2016 14:49:31

Katika hali ya kushangaza mahakama ya wilaya ya Kisarawe imemuhukumu kifungo cha mwaka mmoja cha nje, Mtuhumiwa PETRO GEMBE kwa kosa la uvamizi na ubakaji iliyokuwa inamkabili akishtakiwa na Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

 Kwa mujibu wa nakala ya hukumu ambayo mwandishi wa habari hizi ameipata, Inadaiwa tarehe 24 Juni mwaka 2015 mtuhumiwaPETRO GEMBE akiambatana na wenzie majira ya saa moja usiku walivamia makazi ya BW.FESTO LOYA kwa nia ovu.

Inasemekana mtuhumiwa huyo na wenzie walipora mifugo ng”ombe 53 na wenye thamani 21,000,000/=  na fedha taslimu shilingi milioni 48,350,000/= ambapo vitu vyote vilivyoporwa vina thamani ya shilingi milioni 69,350,000/=  mali ya BW. FESTO LOYA ikiwa pamoja na kuondoka na mkewe DANGA’U GEIDA na kuishi naye kama mke bila idhini yake.

BW.LOYA amebainisha akiwa mkazi wa kijiji cha Kimalamisale amesikitishwa na hukumu hiyo iliyotolewa na hakimu mkazi  wa mahakama ya wilaya ya Kisarawe BW. HAMIS SALUM kwa sababu haki haijatendeka kwani kosa la uvamizi ,uporaji na ubakaji wa Mkewe hakiwezi kulingana na hukumu ya kifungo cha nje mwaka mmoja.

Na ameitaka mahakama kutoa haki na sio kuuza haki kama ilivyojidhirisha katika kesi hiyo, kwani kwa kufanya hivyo baadhi ya wananchi wam ekuwa wakipoteza haki zao kutokana tu na umaskini hata kama wakiwa wao ndio wana haki.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA