VIDEO-KIKONGO WALALAMIKA KUHUJUMIWA MAPATO YAO NA HALMASHAURI YA WILAYA KIBAHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/21/05/2016 10:43:00

Wananchi wa Kata ya Kikongo wamelalamikia halmashauri ya wilaya ya Kibaha kusitisha uchimbaji wa madini ya mchanga ambao ulikuwa unaipatia Kata hiyo mapato na kutoa fursa hiyo kwa mtu binafsi.

Mwenyekiti wa zamani wa serikali ya kijii cha Kikongo, BW. JUMA JUYA amesema kuwa akiwa katika hiyo  amesema akiwa mkusanyaji wa fedha za   mchanga ikiwa pamoja na kuwasomea mapato na matumizi na wakawa wanaenda sawa na wananchi.

BW.JUYA ameongeza makusanyo ambayo yalikuwa yanapatikana yalitumika katika shughuli mbambali za maendeleo ikiwa pamoja na kutoa ajira kwa vijana zaidi ya hamsini ambao waliweza kujikimu kimaisha.

Naye BW. SALUM SAID amesema kuwa wamestuka kwamba mapato ya kijiji ya yanahujumiwa kutokana na wananchi kuamua kuunda kamati ya muda ya kusimamia shimo hilo ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja wa kamati ya muda iliweza kukusanya takriban shilingi milioni 3.5 na hivyo kuweka wazi mapato ambayo yalikuwa yanaishia mifukoni mwa wachache.

Baada ya halmashauri ya Kibaha kuona wananchi wamechukua hatua ya kusimamia machimbo yao wenyewe waliamua kusimamisha uchimbaji wa mchanga na kumtafuta mkandarasi binafsi wa kuchimba mchanga huo na kukiacha kijiji hakina mapato.

BW. SAID ameitaka TAMISEMI kuainisha vyanzo vya mapato vya halamshauri na vyanzo vya mapato ya kijiji ili kuepusha mkanganyiko ambao unalenga katika maslahi binafsi zaidi.

Juhudi za kuonana na viongozi wa halmashauri ya wilaya Kibaha ili kutoa ufafanuzi ziligongwa mwamba ikiwa pamoja na kuwasiliana nao kwa simu na Afisa mazingira, BIBI ANNA MULEBA na Mkurugenzi TATU SELEMAN ambao muda wote hawakutoa ushirikiano stahili.


END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA