MEI 23 SIKU YA FISTULA ULIMWENGUNI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/22/05/2016 09:53:51
Maadhimisho ya
siku ya Fistula ambayo yanatarajiwa kufanyika Mei 23 mwaka huu Mashirika
yanapambana na tatizo hilo nchini yamelenga katika kuhakikisha wanafanya kazi
kwa karibu na vyombo vya habari ili kuweza kufikisha elimu juu ya ugonjwa huo
kwa jamii.
Mwakilizi msidizi
wa shirika la Umoja wa Mataifa UNFPA nchini, BI. CHRISTINE MWANUKUZI KWAYU
amesema kwa kushirikiana na vyombo vya habari kutawezesha wanawake wanaoishi na
tatizo la Fistula kujitambua na kuchukua hatua sthahili.
BI. KWAYU
amebainisha kuwa takriban wanawake milioni mbili wanaishi na tatizo hilo
ulimwenguni na inakadiriwa wanawake takriban 800 wanafariki dunia kwa tatizo la
fistula kwa mwaka.
Aidha amefafanua
Mwakilishi msaidizi huyo wa UNFPA nchini, BI. KWAYU kuwa athari ambazo
zinawapata wagonjwa hao ni pamoja na kunyanyapaliwa na jamii kutokana na hali
ya kutokwa haja bila kujitambua.
Akizungumzia
kuhusiana na kundi ambalo linapata kwa kiasi kikubwa tatizi hilo ni wasichana ambao wanabeba mimba za utotoni,
hatua ambazo UNFPA imezichukua mpaka sasa ni kutoa elimu ya kwa wahudumu wa
afya 4000 na kutoa usaidizi katika masuala ya uzazi wa mpango.
BI. KWAYU
ameitaka jamii kuwapeleka watoto wa kike shule ili kuwaepusha na mimba za
utotoni ambazo ndio chanzo kikubwa cha ugonjwa wa fistula kwa kinamama.
Mashirika mengine
ambayo yanaunganisha nguvu katika kupambana na tatizo la Fistula ambalo
linasemekana kuwa korofi katika maeneo ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na
Asia ni CCBRT, AMREF kwa kutoa usaidizi tofauti ili kuweza kushinda tatizo
linalowezekana kumalizwa kabisa.
END
Comments
Post a Comment