WALAMIKIA MALIPO KIDUCHU HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/7/28/2014
6:16:35 PM
Watumishi wa
kitengo cha mazingira halmashauri ya mji wa Kibaha wameendelea kulazimika
kufanya kazi kwa kima cha mshahara wanacholalamikia ambacho wao hawakubaliani
nao.
Mwandishi wa
habari hizi amewashuhudia watumishi hao wakifanya kazi hiyo jana ikiwa ni
sehemu ya wajibu wao kuhakikisha kuwa nji wa Kibaha unakuwa safi muda wote
sambamba na uwepo wa gari la kisasa la taka.
Nimebahatika
kuongea na watumishi hao wa mazingira ambao walikuwa na mambo kadhaa ya
kuelezea, Mmoja wa BW.KASSIM MALIVI amesema wao wanalipwa shilingi 125,000/-
kiwango ambacho hakitoshelezi mahitaji na kulinganisha na uzito wa kazi
wanayofanya.
BW.MALIVI ameongeza wamepeleka malalamiko yao sehemu
mbalimbali wakitaka kuboreshewa maslahi yao, Hatua ambyo iliwafikisha hadi
ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kibaha BI.HALIMA KIHEMBA ambaye aliaahidi
kulishughulikia suala hilo kwa karibu.
Naye mtumishi
mwingine BW.JUMANNE KADALA amesema kuwa yeye anaipenda kazi yake na kuna kitu
kidogo kinachomkwaza ambacho ni kiwango kidogo cha malipo wanayopewa na
halmashauri.
BW.KADALA
ameenda mbali na kuiomba halmashari kuwaongezea mshahara hadi kufikia shilingi
laki moja themanini za Kitanzania, ili waweze kujikimu na hali ngumu ya maisha
inayowakabili watanzania walio wengi.
Mwandishi wa
habari hizi alipoongea kwa njia ya simu na Mkuu wa wilaya ya Kibaha kuhusiana
na suala hilo, alikiri kulifahamu na tayari ameshalifanyia kazi kwa kuwasiliana
na Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha kwa ufumbuzi.
END.
Comments
Post a Comment