WAJASIRIAMALI WAPONGEZWA KIBAHA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/4-07-2014
Vikundi vya ujasiriamali katika Kata ya Kibaha, mjini
Kibaha wamepongezwa kwa kuweza kuvipatia vikundi vyao mafanikio kufuatia
kuwezeshwa na mke wa Mbunge wa Kibaha mjini, BI.SELINA KOKA, shilingi laki tatu
kwa vikundi sita vya wajasiriamali.
Akitoa pongezi hizo Mke wa Mbunge wa Kibaha, BI.SELINA
KOKA amesema ametiwa moyo na vikundi hivyo vya kinamama ambavyo alivipatia
mitaji midogo ya takriban shilingi laki tatu kwa kila kikundi ili kuviwezesha
kutimiza ndoto zao angalau kwa kiasi Fulani.
BI.KOKA amebainisha kuwa kikundi cha wajasiriamali cha
Mzabibu kimemfurahisha kwa kuweza kufanya mambo mkubwa kiasi cha kuweza kununua
pikipiki kufuatia rfedha ambazo alizowapatia.
Ameongeza kuwa kutokana na juhudi zilizoonyeshwa BI.KOKA
anatoa shilingi laki moja kama motisha kuongezea pale ambapo alitoa awali na
kuviongezea uwezo vikundi hivyo ambavyo kwa kiasi kikubwa vinahusisha kinamama.
Katibu wa UWT Kata ya Kibaha,BI.SADADUDA MADENGE
amemshukuru BI.SELINA KOKA kwa misaada yake mbalimbali anayotoa kulenga makundi
tofauti ya kijamii na hususan kinamama, na kuita kitendo hicho ni sawa na
kugawana anachopata Bungeni na wananchi wake kulinganisha na waliomtangulia.
BI.MADENGE amemtaka mke wa mbunge kuendelea na moyo
huyohuo wa kuwajali watu wa kawaida katika jamii.
END.
Comments
Post a Comment