LIGI YA DARAJA LA NNE KUANZA KIBAHA.
Ben
Komba-Pwani-tanzania-10/07/2014
Ligi daraja
la nne wilaya ya Kibaha inatarajiwa kuanza mara baada ya kukamilika mwezi
mtukufu wa Ramadhani, kama kalenda ya michezo ya chama hicho inavyoonyesha.
Mwandishi wa
habari hizi akiongea na Katibu wa chama cha soka wilayani Kibaha, SEIF KIDODO
amesema fomu kwa ajili ya kujiandikisha kushiriki ligi hiyo ya daraja la nne
zimeshaanza kutolewa kwa timu ambazo zina lengo la kushiriki ligi hiyo.
KIDODO ameongeza
kuwa kila timu italazimika kulipa kiasi cha shilingi 30,000 ikiwa ni ada ya
kiingilio ambayo itatumika katika masuala mbalimbali ya uendeshaji wa ligi
hiyo.
Zaidi Katibu
wa KIBAFA anaongeza kuwa mwisho wa zoezi hilo ni tarehe 22 Julai mwaka huu.
END
Comments
Post a Comment