WAZEE WANYANGANYWA MASHAMBA NA VIJANA BAGAMOYO




Ben Komba/Pwani-Tanzania/`08-07-2014
Wazee wanaoishi vijijini wanakabiliwa na hatari kubwa ya kunyang’anywa maeneo na baadhi ya vijana ambao wana tamaa ya kujitajirisha kwa kuwasumbua wazee hao, huku wakidai maeneo ambayo wameishi miaka yote ya maisha yake kuporwa na vijana.
Mmoja wa waathirika wa tukio hilo,Mkazi wa Msata Madesa wilayani Bagamoyo, Hakimu mstaafu, BW.PATRIC MBENA TANGA kukumbana na dhahama hiyo ambayo inampa wakati mgumu katika ufuatiliaji wa suala hilo kutokana na utu mzima alio nao.
BW. MBENA TANGA amebainisha kuwa yeye alihamia  eneo la Msata Madesa kufuatia operesheni vijiji ya mwaka 1970 ambayo ilikuwa inahimiza wananchi wakae katika vijiji vya ujamaa kwa lengo la kutoa huduma kwa urahisi kwa wananchi.
BW.MBENATANGA ambaye kwa sasa anakaribia miaka 102 amesema kuna baadhi ya watu ambao amehamia nao kutoka kijiji cha mashambani cha Mkambarani ambako alikuwa na mashamba pamoja na wenzie ambao leo hii wapo hai.
Lakini cha kushangaza miaka ya hivi karibuni kulijitokeza, BINTI.MARIA GONZA na kudai eneo la hilo la mzee MBENATANGA ni lake, Na Baraza la usuluhishi la kijiji cha Msata Madesa likatoa maamuzi ya eneo hilo ni mali halali ya Mzee PATRICK MBENATANGA.
Lakini cha kushangaza anayedaiwa mvamizi alikata rufani baraza la usuluhishi la kata la Msata ambao nao wakatoa uamuzi bila kushirikisha mashahidi wa awali ambao walitoa ushahidi kijijini, na kumnyang’anya Mmiliki halali eneo lake na kumpatia mvamizi.

Baadhi ya wazee ambao waliishi pamoja na mlalamikaji, BW.RAMADHANI MWASSA amesema kinachoendelea ni utamadun i uliozuka kwa baadhi ya vijana kupora maeneo ya wazee wazima wakishirikiana na baadhi ya watumishi wasio waaminifu katika baraza la kata kuwapora mashamba wazee kwa l;engo la kuyauza hususan wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Bw.Mwassa ameongeza anavyofahamu yeye eneo hilo ni la mlalamikaji na ndio maana baraza la usuluhishi la kijiji halikupata tabu kutoa uamuzi kuhusiana na suala hilo, ndipo MARIA GONZA alipokata rufaa kung’ang;’ania eneo ambalo hata baba yake mzazi kasema hawahusiki nalo.

Inasemekana katika baraza la kata, BI.MARIA GONZA alitoa shilikingi laki moja unusu kwa ajili ya baraza la kata ambalo nalo lilitengua hukumu ya kijiji na kumkabidhi shamba hilo mvamizi.

Nikiongea na Msaidizi wa Kisheria kutoka KIBAHA PARALEGAL CENTRE, ambayo ipo chini ya WLAC MWL.SAMUEL RUHEMBE amesema kuwa wazee watu wazima wanakabiliwa na kitisho kikubwa kutoka kwa vijana ambao wamekuwa wakikata mashamba yao na kuyauuza bila kushirikisha wamiliki, ameishauri serikali kutupia macho suala hilo, ikiwa pamoja na kufuatilia kwa karibu utendaji kazi wa mabaraza ya ardhi na nyumba ya kata, kwani yamekuwa kama muhuri wa kunyang’anya haki za wanyonge.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA