SHIRIKA LA ELIMU LAKABILIWA NA UKATA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-07-2014
Shirika la elimu Kibaha lipo katika changamoto kubwa ya kukabiliana na mahitaji ya hospitali iliyo chini yake kutokana na kukosekana kwa rasilimali fedha za kutosha kuweza kuwalipa wauuguzi stahili zao kama sheria za kazi zinavyoelekeza.
Mkurugenzi wa Shirika la elimu Kibaha BW.CYPRIAN MPEMBA ameyazungumza hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi hospitalini hapo, amesema yeye kwa upande wake hana mtima nyongo na mtumishi yoyote linapokuja suala la maslahi yao.
BW.MPEMBA amewahakikishia wauguzi kuwa waandike mapendekezo yao na kuyafikisha ofisini kwake ili kuweza kuyapitia na kuyafanyia kazi na hasa ikizingatiwa kuwa wauuguzi wanakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na kuwa wachache kufuatia kustaafu kwa waliotangulia.
Mkurugenzi huyo wa Shirika la elimu Kibaha BW.MPEMBA ameongeza kuwa hauwezi kuzungumzia maendeleo iwapo viashiria vya afya vina tatiza, na kwa uwepo wa wauguzi kunasaidia kuharakisha maendeleo kutokana na afya ya wananchi kuimarika.
Awali akisoma risala katika siku hiyo BI.PREDICANDA SIMTOWE amesema kauli mbiu "WAUUGUZI NI NGUVU MUHIMU YA MABADILIKO RASILIMARI MUHIMU KWA AFYA" na malengo waliyojiwekea ni kuhakikisha uwepo wa huduma ya uzazi salama inatolewa kwa uhakika na kuzingatia bora,kushirikiana na Wizara ya afya katika kuhakikisha wanapunguza maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI, na kutokomeza malaria na kuelimisha wazazi kuzingatia chanjo na kupunguza vifo vya watoto wa umri ya chini ya miaka 5.
BI.SIMTOWE ameongeza kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, ikiwa pamoja upungufu wa vifaa vya kutendea kazi na hasa ukizingatia kuongezeka kwa wagonjwa, upungufu wa mashuka na vifaa vingine muhimu kwa kazi zao.
END.
Comments
Post a Comment