CHAMAKWEZA WALILIA SOKO LA MAZIWA



Na Omary Mngindo, Bagamoyo
Julai 4

WANAWAKE jamii ya wafugaji katika kijiji cha Chamakweza Kata ha Pera
Bagamoyo Pwani wanaiomba serikali kuwajengea soko la kuuzia maziwa kwa
lengo la kuendeleza biashara zao na hatimaye kujikwamua kiuchumi.

Wakizungumza kijijini hapo juzi, wakazi hao Bi. Husna John na Maria
Mika walisema kuwa pamoja na kujihusisha na uuzaji wa biashara hiyo ya
maziwa lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa soko hali
inayowafanya wauze kwa bei ya kutupa na wakati mwingine kuwakopesha
watu ambao hawawafahamu.

"Sisi wanawake jamii ya wafugaji tunajihusisha na biashara ya kuuza
maziwa lakini hatuna soko la kuuzia hivyo tunaiomba serikali itujengee
soko kwa ajili ya kuuzia maziwa au kututafutia soko la uhakika la
bidha hiyo ili tujikwamue kiuchumi," alisema Husna.

Naye Maria alisema kuwa kutokana na kukosekana kwa soko hilo
wanalazimika kuuza lita moja kwa sh. 500 bei ambayo kimsingi haina
faida ukilinganisha na gharama wanayoitumia katika kuwatunza ng'ombe
jambo ambalo limekuwa likisababisha hasara kubwa kwa wanawake hao.

"Tunalazimika kuwakopesha watu wanaotoka jijini Dar es Salaam  ambao
baadhi yao si waaminifu hivyo kuondoka na fedha zetu na kusababisha
hasara kubwa kwetu ukilinganisha na gharama tunazozitumia katika
kuwatunza ng'ombe hao," alisema Maria.

Kwa upande mwingine wakazi hao wameomba mradi wa maji unaoendelea
kusambazwa kijijini hapo ufikishwe pembezoni mwa vijiji ili kuwasaidia
waliowengi ambao wanaishi maeneo hayo mbao wanatumia maji katika
malambo ambayo yamebomoka kufuatia mvua zilizonyesha hivi karibuni.

"Huu mradi wa maji unaonedelea haopa kijijini tunaiomba serikali
ielekeze nguvu zaidi pembezoni ambao ndiko tuankoishi tuloweni ambapo
tunategemea mai kupitia malambo ambayo yamebomoka kufuatia mvua
zilizonyesha miezi michace iliyopita," alisema mkazi huyo.

MWISHO.

WAKAZI KONGOWE WALIA KUPUUZWA KWA AGIZO LA JK

Na Omary Mngindo, Kibaha
Jula 4

WAKAZI wa Kata ya Kongowe Kibaha mkoani Pwani wanaendelea na kilio cha
kupuuzwa kwa agizo lililotolewa na Rais Jakaya Kikwete alilolitoa
Oktoba mwaka 2010 katika kampeni ya kuwania nafasi hiyo.

Wakazi Hamisi Mgobanya na Mwinyimvua Viziwa waliyasema hayo juzi
wakazi wananzungumza na waandishi wa habari Kongowe ambapo walielezea
masikitiko yao kutokana na kupuuzwa kwa agizo lililotolewa na Rais
Kikwete alilolitoa kwenye kampeni hiyo mbele ya maelfu ya wakazi hao
ambao wanalilia barabara ya Kongowe kupitia Misitu kutokea Yombo
kuelekea Bagamoyo.

"Tunashangazwa kuona viongozi wa halmashauri mbili za Kibaha na
Bagamoyo kupuuzia agizo lililotolewa na kiongozi wao wa ngazi za juu
tena Rais alilolitoa mwaka 2010 kwenye kampeni hapa Kongowe la kutaka
kufunguliwa kwa barabara inayotokea Kongowe kupitia Misitu kutokea
Yombo na kuelekea Bagamoyo, tangu litolewe mpaka sas miaka minne
halijafanyiwa kazi," alilalama Mgobanya.

Aliongeza kuwa kwa miaka zadi ya kumi sasa wakazi wa wilaya hiyo
wanapotaka kwenda Bagamoyo hulazimika kupitia jijini Dar es Salaam au
Mlandizi jambo ambalo linawatia majonzi makubwa kwani barabara hiyo ni
ya mkato na isitoshe hata nauli yake ni nafuu ukilinganisha na
mzunguko huo.

"Nashangaa kuona wabunge wetu wawili wa jimbo la Kibaha Mjini Koka
Silvestry na Shukuru Kawambwa wa Bagamoyo kushindwa kuwa kimya katika
utekelezaji wa agizo la mkuu wao, hii inaonesha picha gani kwa
wananchi wa kawaida?, alihoji Mgomanya.

Kwa upande wake Viziwa alisema kuwa hali hiyo inawatia doa viongozi
hao wanaoaminiwa na wananchi tena isitoshe ndio wanaokiongoza chama
ambacho kinashika dola katika nchi na kuhoji inakuwaje viongozi hao
wanapuza agizo la rais?

"Kwa kweli jambo hili linauma sana kwani linatuacha katika mazingira
ambayo hatupati ibu la usahihi nani kati ya rais na viongozi wa
halmashauri, kwa maana Kikwete alitoa agizo la kutaka kufunguliwa kwa
barabara hii laini mpaka leo tunavyozungumza na vyombo vya habari ni
miaka minne sasa hakuna dalili zozote," alisema Viziwa.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA