MWENGE WA UHURU WAINGIA PWANI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/222-07-2014/10:20
Mbio za Mwenge uhuru
umeingia katika Mkoa wa Pwani ukitokea mkoani Lindi ambako umemaliza mzunguko
wake kwa kukagua, kuweka mawe ya msingi na kufungua miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Mwenge huo
ulikabidhiwa kwa Kaimu Katibu tawala,BI.SIMFROZA MMARI kutoka kwa Afisa Tawala
wa Mkoa wa Lindi BW.ABDALLAH CHIKOTA, katika kijiji cha Kiwanga wilaya ya
Rufiji mpakani mwa Mkoa wa Pwani na Lindi.
Akiongea mara baada
ya kupokelewa kwa Mwenge huo,Kaimu mkuu wa Mkoa wa Pwani, BI.HALIMA KIHEMBA
amesema kuwa Katika mkoa wa Pwani mwenge unatarajiwa kufungua, kuweka mawe ya
msingi na kuzindua miradi inayokadiriwa kufikia bilioni 15 na kati ya miradi
hiyo wilaya ya Rufiji pekee ina miradi inayogharimu bilioni 5.
Akizungumza katika
sherehe hiyo ya makabidhiano ya Mwenge wa uhuru, Kiongozi wa mbio hizo kitaifa,
BI RACHEL KASSANDA alitumia nafasi hiyo kukemea vitendo vya mauaji ya wanawake
yanayoendelea katika wilaya ya Nachingwea.
BI.KASSANDA amemtaka
Mkuu wa Mkoa wa Lindi BW.LUDOVICK MWANANZILA kulivalia njuga suala hilo ambalo
limekuwa likiwapa wasiwasi na mashaka makubwa kinamama wilayani Nachingwea
kutokana wenzao kukutwa wameuwawa na kukatwa maeneo ya siri ikiwa pamoja na
kutmbukizwa vjiti.
Moja ya miradi
iliyofunguliwa ni Mradi mkubwa kabisa ambao umegharimu shilingi Bilioni 4.5 ni
Mradi wa kilimo na Kiwanda cha kusindika muhogo katika Kata ya Bungu wilaya ya
Rufiji mkoa wa Pwani, mradi huo ambao unatarajiwa kugharimu dola za kimarekani
milioni 10 utakapokamilika ambazo ni sawa
na shilingi bilioni 16 za Kitanzania.
Mkurugenzi wa huduma
za jamii wakiwanda hicho, BW. DEONATUS MALEGESI amesema uwezo uwezo wa kiwanda
hiki kidogo ni kusindika tani 60 za muhogo mbichi kwa siku moja na kutoa tani
12 za wanga kwa maana hiyo mahitaji hali ya ni tani 20,000 za muhogo kwa mwaka
ambazo zitatoa tani 3600 za wanga.
BW.MALEGESI ameongeza
kuwa kampuni itakuwa inanunua muhogo wenye thamani ya shilingi za kitanzania
bilioni2 kwa mwaka kwa kiwanda kidogo na bilioni 12 kwa kiwanda kikubwa.
END.
Comments
Post a Comment