WENYE MABUCHA WAGOMA KUUZA NYAMA MJINI KIBAHA VIDEO


Ben Komba/Pwani-Tanzania/19-07/2014

Wafanyabiashara wa mabucha mjini Kibaha wamegoma kufanya shughuli hiyo kufuatia halmashauri ya mji wa Kibaha kuwahamisha kutoka machinjio ya awali na kuwapeleka katika machinjio mpya ambayo hawakuridhika nayo kutokana na kukosekana kwa miundombinu ya kutosha.


Msemaji wa wafanyabiashara aliyejitambulisha kwa jina la BW.ATHUMAN MKANGA amesema wao wameamuamua kuchukua uamuzi huo kufuatia halmashauri kutoa tamko la lazima ambalo linawataka wao kuhamia eneo hilo na hawatarusiwas tena kuchinja katika machinjio hayo ya zamani.


Msemaji huyo amesema kuwa wao hawakatai kuhamia katika machinjio hiyo inayoitwa ya kisasa kwa sababu miundombinu yake bado haijakamilika na hata mvua ikinyesha ina uwezekano mkubwa kulowesha nyama na hivyo kupoteza Thamani halisi.


Aidha BW.MKANGA amebainisha kuna tatizo kubwa la maji ikiwa pamoja na kukosekana kwa umeme wa uhakika, na hivyo kuweza kusababisha nyama zao kuharibika na ng'ombe kuweza kutorokea porini kutokana na machinjio hayo kupakana na FOREST na Jeshi na ilihali hakuna wigo uliiojengwa kuzunguka machinjio.


Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BI.JENIFA OMOLO alipopigiwa simu ili kutoa ufafanuzi kuhusiana na suala hilo anasema anachojua yeye machinjio ya kisasa imeshakamilika nas ni juu ya wafanyabiashara wa mabucha kuhamia huko.


Ameongeza halamshauri itayafanyia kazi mapungufu ambayo yamejitokeza ili kuwezesha machinjio hayo ya kisasa kabisa kuweza kutumika.


Machinjio hayo yameigharimu halmashauri zaidi ya shilingi milioni 60 za Kitanzania


END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA